Job Ndugai ni Naibu spika wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania lakini pia ni mjumbe kwenye bunge la katiba na pia mwenyekiti wa kamati namba 8 kwenye bunge la katiba.
September 12 2014 aliwasha kipaza sauti bungeni na kusema > ‘Nimesimama hapa, nitakayoyasema ni yangu mwenyewe na sio yale ya kamati’
- Ingekua ni vema kama mchakato huu wa katiba mpya ungemalizika katika kipindi hikihiki ambacho Rais Kikwete ni Rais, sababu yeye ndio muasisi wa jambo hili…. wako wanaoshangilia kwamba iende 2016, unampangiaje Rais ajaye vigezo vya vipaumbele vyake? ukishaanza kuweka viraka kwenye katiba ya mwaka 1977 sasa una haja gani ya katiba mpya?
-
Kwenye chama cha mapinduzi tumeahidi kwamba tuaendelea na serikali
mbili zilizoboreshwa, kwenye zilizoboreshwa hapa mapendekezo yangu ni
kwamba Mabunge yabakie mawili, baraza la Wawakilishi na bunge la
Jamuhuri lakini bunge la Jamuhuri liwe na ajenda mbili za kudumu, mambo
ya muungano na yasiyokuwa ya muungano.
3. Yamekuwepo malalamiko ya Zanzibar kuhusu mafuta na gesi kwamba itoke katika orodha, kwa sababu wenzetu ni Wadau mi nafikiri jambo hilo liwe hivyo japo ukiniuliza mimi ningependa libaki.
- Kuhusu utawala, Mh. Rais amepewa madaraka na mamlaka kadhaa ya kuwa na uteuzi mbalimbali wa kufanya, ushauri wangu ni kwamba pale alipopewa nafasi ya uteuzi vilevile apewe nafasi ya kutengua uteuzi wake, kwanini nasema hivyo? wako watu walioteuliwa na Mh. Rais lakini ndio wanaopita huko kumpinga kila kukicha.
No comments:
Post a Comment