Baadhi ya majeruhi wa ajali ya moto wakiwa wodini.
MAJERUHI 9 kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali
ya Taifa Muhimbili baada ya kuungua na moto uliosababishwa na kuungua
kwa lori la mafuta huko Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka
huu, wanaendelea na matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.
Kamera yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao
wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji
na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi
sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.
Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya
zaidi ambao aliwataja majina yao kuwa ni Mathayo Danie (21) na Hamis
Ally (35).
Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu
kuchota mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni
Abbas Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21)
Hamis Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki
Martin.
No comments:
Post a Comment