Vijana
wenye ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi wamepatiwa mafunzo ya wiki moja
nakukamilisha sehemu ya kwanza ya mafunzo wanayohudhuria mara mbili kwa mwaka
ambapo wamejifunza Ujasiriamali, Kilimo Jikoni, Elimu yauzazi, Kujamiina pamoja
na msongo wa mawazo, mafunzo hayo yalifanyika jumatatu tarehe 28/04/2014 nakumalizika tarehe 2/05/2014 CCBRT - Moshi Mkoani
Kilimanjaro.
Mratibu
na kiongozi wa shughuli za vijana wenye ulemavu wakichwa kikubwa na mgongo wazi
Bw. Shadracky Domingo amekuwa akifuatilia kwa makini mafunzo hayo na kujifunza
nao lengo ikiwa nikutakakufahamu namna walemavu wanavyoweza kuzitumia fursa
watakazo ambiwa na wakufunzi, amesema kwa mujibu wa mafunzo anahakika ikiwa
vijana hao watajiamini na kuwa na uthubutu watafanikiwa.
Mmoja
wa vijana walioshiriki mafunzo Bw. Emmanuel Lymo ametoa ushauri wake nakusema
“walemavu wanatakiwa kujikubali, kuwa wenyekuamua na kutenda” aliongeza kusema
kuwa ulemavu haidhuru kuwa na mafanikio, alimalizia kwakusema wapo watu wengi wenye
ulemavu ni maarufu, wakiwemo viongozi wa nchi, na wengine wataalamu wa
teknolojia wanamaendeleo na mafanikio makubwa, kwao watu hao ingefaa kuwa mfano
wa kuigwa.
Mkufunzi
wa ujasiriamali Bw. Issac Ara wakati yeye akihitimisha mafunzo yake aliwataka
vijana kuamua kuthubutu, kujiamini na kuwa wenye malengo timilifu. Akielezea
sifa za mjasiriamali aliwashirikisha kila mmoja katika kumtaka aeleze ni
namnagani anaelewa tofauti za mjasiriamali na ujasiriamali, pia aliwaeleza
fursa walizonazo ni nyingi hivyo nikujiamini na kuchukua hatua.
Vilevile
alifundisha kuwa kwakila wazo yafaa kuliweka kwenye uso wa karatasi,
akimaanisha kuliandika lile mtu unaloliwaza
kufanya, au umiliki kama mradi, biashara ama taasisi. Pia alieleza namna
yakuandaa wazo, kuliweka katika uso wa karatasi, kuandika na kuweza kuwa
biashara kamili yenyekuingiza kipato. Bw. Ara alimalizia kwakumkaribisha
mwenyeji na mratibu wa mafunzo ya vijana hao Bw. Domingo ilikuweza kuhitimisha
shughuli hiyo.
Bw.
Domingo aliwataka vijana kutoa maoni yao kwakilewalichojifunza, pia aliwapa
fursa ya kuchagua aina mpya ya mafunzo ambayo wangehitaji kuyapata katika awamu
ya pili watakaporudi tena mwezi wa (12) Disemba mwaka huu. Aidha kila mmoja
aligawiwa mbegu za mbogamboga ili kwenda kuotesha kwao, ikiwa kama sehemu ya
mafunzo ya vitendo ya kilimo darasani.
Wawezesha wa mafunzo ya wiki ya vija wenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja. |
No comments:
Post a Comment