NAIBU WAZIRI WA FEDHA AWATUNUKU VYETU
WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA WALIOHITIMU MASOMO YA MIPANGO
MIKAKATI(SADC & EAC)
Naibu
Waziri wa Fedha akisalimiana na Wahadhiri wa Chuo Cha Uhasibu Arusha
mara baada ya Kuwasili tayari kwaajili ya Kuongoza Mahafali ya Kwanza ya
Wanafunzi wa Kutoka Nchi za SADC na EAC waliokuwa wanasomea kozi za
Masomo ya Strategic Programmes.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiwa kwenye Matembezi ya pamoja na
Wahitimu kuelekea eneo la Mahafali katika Ukumbi wa Chuo cha
IAA,Matembezi haya yaliongozwa na BlassBand ya Jeshi.
Mh.Mwigulu
Lameck Nchemba akizungumza na Wahitimu Pamoja na Wahadhiri namna
alivyofurahishwa na Fursa hii ya Kuimarisha Umoja wa Nchi zetu za SADC
na EAC kupitia Elimu,Pia Ubunifu Uliofanywa na Chuo Cha Uhasibu Arusha
kuruhusu Masomo ya Mipango Mikakati kwaajili ya Maendeleo ya Jumuia
Zetu.
Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akiwatunuku Vyeti Wahitimu.
Baadhi
ya Wahitimu wa Diploma-Post Graduate in Strategic Programmes wakivaa
Kofia zao ikiwa ni Ishara ya Kuheshimu tunuku ya Elimu yao kutoka kwa
Naibu Waziri wa Fedha.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiwa katika Picha ya Pamoja na
Wahitimu wa Masomo ya Mipango Mikakati katika ngazi ya Ordinary Diploma
na Post-Graduate Diploma Chuo Cha Uhasibu Arusha Jana tar.12/03/2014
mara baada ya Kuwatunuku Vyeti.Wahitimu ni Wanafunzi kutoka Nchi za
Southern Africa Development Community(SADC) na East Africa
Community(EAC) Picha na Sanga Festo
CHANZO:FRANCI GODWINBLOG
No comments:
Post a Comment