TTCL

EQUITY

Thursday, January 2, 2014

MREMBO AVUA NGUO KWA SHEMEJI YAKE KUFUMANIWA....

kweli dunia uwanja wa fujo! Mrembo aliyetajwa kwa jina la Baby amefanya kituko cha aina yake kwa kusaula nguo mbele ya hadhara baada ya shemeji yake maarufu kwa jina la Baba K kufumaniwa.
 

FUMANIZI LAIVU

Tukio hilo la aina yake lililovuta wengi lilijiri kwenye gesti moja (jina tunalo), maeneo ya Temeke jijini Dar hivi karibuni baada ya jamaa mmoja kumwekea mtego rafiki yake aliyekuwa akimtongoza mkewe na kumfumania laivu.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mara baada ya fumanizi hilo, mrembo huyo ambaye ni shemeji wa mwanaume aliyefumaniwa alionesha maajabu alipoamua kuvua nguo bila kusitasita.

 

“Alianza kuvua kidogokidogo, baadaye akaamua kuvua zote na kubakia na nguo ya ndani tu. Kwa kweli iliwashangaza wengi pale kwenye eneo la fumanizi. Halafu unajua fumanizi lenyewe lilikuwa ndani ya chumba, dada yake alikuwa huko, yeye nje,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Imeelezwa kuwa, baada ya mwanamke huyo kuvua nguo  alianza kushangilia kwa nguvu huku akirukaruka kwa furaha na kusema:

“Heee! Mwanaume kapatikana leo, kwa furaha namwaga lazi, eti shemeji. Shemeji gani unamwacha mkeo unakwenda kwa vidampa?”


 

AKATA MAUNO
Ilielezwa kuwa furaha ya mwanadada huyo haikuishia katika kuvua nguo na kusema hivyo tu, kwani aliendelea kusheherekea kwa kukata mauno huku na kule kama anayetamba.


Ilisemekana kwamba wakati ‘akifanya yake’ midume na watoto walikuwa wakifaidi sinema ya bure huku wengine wakiona aibu na kujichomoa zao eneo la tukio.


“Labda anamshukuru Mungu kwa kufanikisha fumanizi la shemeji yake kwa kuwa alihusika kwenye kusuka mchezo mzima,” alisema shuhuda mwingine.

 

MSHANGAO

Kitendo hicho cha kusaula nguo zote na kushangilia kiliwashangaza baadhi ya watu ambao walikuwepo eneo hilo la tukio na wengi wao wakajiuliza kulikoni shemeji mtu apitilize furaha kiasi hicho kisa tu mume wa dada yake kafumaniwa?


Wakizungumza na Paparazi wetu, mashuhuda hao walisema kwa vyovyote kuna la ziada nyuma ya pazia ndiyo maana mwanadada huyo alifurahi kupita kiasi.


“Kwa vyovyote kuna kitu, si bure. Mbona huyu dada kapagawa kuliko hata aliyefumania? Mh! Yetu macho,” alisema mmoja wao huku mwingine akidakia:

“Hapa dada mtu anatakiwa kuwa makini sana na huyu dada si ajabu anachochea ili ndoa ivunjike achukue nafasi. Hawa ndiyo akina dada wa mjini bwana.”


 

MSIKILIZE ASEMAVYO

Paparazi wetu alipomvaa mrembo huyo na kumuuliza kwa nini alikuwa amepagawa na kusaula nguo, mwanadada huyo alijibu kwa mkato kuwa alifurahishwa mno na fumanizi hilo ingawa alikiri aliyefumaniwa anaumia huko alipo.


Hahahahaaa…Huyu shemeji yangu amezidi, afadhali leo amefumaniwa nimefurahi sana,” alisema dada huyo huku akikatiza mtaani akiwa na kufuli pekee.

TURUDI KWENYE FUMANIZI

Katika fumanizi hilo ambalo lilikuwa la aina yake ilielezwa kuwa shemeji mtu alikuwa akimsumbua mke wa rafiki yake ndipo mke huyo akaamua kumweleza mumewe ambaye walimwekea mtego na kufanikisha kumnasa laivu.


Hata hivyo, mfumaniaji na mfumaniwa, wote walikubaliana ambapo jamaa aliyefumaniwa alipewa kibano na onyo kali iwe mwanzo na mwisho kusarandia wake za watu.

Ilidaiwa kuwa, baada ya makubaliano hayo, mambo yote yaliishia hapo bila kufika kituo chochote cha polisi.

-Gpl 

No comments:

Post a Comment