TTCL

EQUITY

Monday, December 30, 2013

USHIRIKINA ...MFIWA ANG'ANG'ANIA KAMBA YA KUSHUSHIA JENEZA LA MAITI AONDOKE NAYO..


 viongozi wa Muungano wa jamii Tanzania[MUJATA]akiwemo Soja Masoko,Abdul Aziz,Diwani Kata ya Mwakibete Lucas Mwampiki na Chifu Shadrack Merere kutoka Mbarali.
Kamaba tayari kwa kuchomwa
 mwenyekiti wa mtaa Bwana Ndongole Mwatebele
akitoa maelezo mafupi kwa machifu 
Chifu Merere alitaka amani katika mtaa huo na kuamua kuiteketeza kamba kwa moto huku umati ukishuhudia tukio hilo na chifu kuahidi kumrejesha kwa mazingara eneo la Mwakibete ili ajibu tuhuma zinazomkabili mtuhumiwa huyo

Imani za kishirikna zimezidi kuchukua sura mpya mkoani Mbeya baada ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Lucy Frank[55]mkazi wa Manyoni Singida kudai kamba iliyotumika kushushia jeneza la marehemu dada yake apewe ili aende nayo Singida.

Kauli hiyo aliitoa katika msiba wa marehemu dada yake aliyefahamika kwa jina la Elizabeth Sibonike[81] aliyefariki ghafla Novemba 19 mwaka huu katika mtaa wa Viwandani kata ya Mwakibete na mazishi yake kufanyika Novemba 21 mwaka huu.

Baada ya mazishi Lucy alidai dada yake kuwa kadhalilishwa kwa kuzikwa kwenye jeneza kubwa na kushushwa kaburini kwa kutumia kamba aina ya manila,akidai vijana walimtuhumu marehemu kuwa ni mshirikina hali iliyomkasirisha.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke Lucy Frank alitamka msibani kuwa yeyote aligusa kamba makaburini atakufa hali ambayo iliwaudhi wakazi wa mtaa huo na kumtaka mwenyekiti wa mtaa Bwana Ndongole Mwatebele kuichukua kamba hiyo na kuitisha mkutano wa hadhara ili mwanamke huyo kutoka Manyoni aeleze umma sababu za kitaka kamba hiyo.

Hata hivyo wananchi wa mtaa wa Viwandani wakitafakari hayo kijana mmoja miongoni mwa waliokamata kamba makaburini  aitwaye Julius Mwandambo alifariki kwa kugongwa na gari eneo la mama John Desemba 15 mwaka huu hali iliyowafanya wananchi kutaharuki.

Wakati taratibu za mazishi zikiendelea Desemba 16 wakati picha ya marehemu ikitembezwa barabarani mtoto wa Lucy alisikika akisema kama aliyefariki ni huyu, bado wengine watafuata hali iliyowafanya vijana kugoma kuchimba kaburi mpaka atafutwe huyo mama na mwanae ili waeleze kauli zao zina mantiki gani.

Katika hali hiyo ya mtafaruku mama huyo na mwanae walienda kuhojiwa kituo cha Polisi kati ambapo mtoto alikiri kutamka maneno hayo ingawa alisema kuwa hakujitambua hivyo anaomba radhi.

Huku wananchi wakimsubiria mwanamke huyo na mwanae kwenye mkutano ilidaiwa kutoroka kwenda Singida na kwamba wananchi hawako tayari kuwaona warudi mtaani hapo.

Mkutano ulioitishwa Desemba 27 mwaka huu ulioitishwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Muungano wa jamii Tanzania[MUJATA]akiwemo Soja Masoko,Abdul Aziz,Diwani Kata ya Mwakibete Lucas Mwampiki na Chifu Shadrack Merere kutoka Mbarali.

Chifu Merere alitaka amani katika mtaa huo na kuamua kuiteketeza kamba kwa moto huku umati ukishuhudia tukio hilo na chifu kuahidi kumrejesha kwa mazingara eneo la Mwakibete ili ajibu tuhuma zinazomkabili

No comments:

Post a Comment