Miaka minne iliyopita msichana huyu
mwenye umri wa miaka 19, Delfina Cedeno, alianza kupata tatizo hili la
ajabu, lililokuwa likimfanya alie na kutoka jasho la damu. Kwa kuongeza zaidi, wakati mwengine damu zimekuwa zikitoka hata kwenye kucha na kitovu.
Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.
Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda
hedhi kwa siku 15 mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu
kutokana na hali hiyo iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi
alivyofanya, madaktari wa mji wake wa Veron, kwenye Jamhuri ya
Dominica, walishindwa kumsaidia.
Cedeno alisema: 'Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri - nilishtushwa na kuogopa.
Anasema alijisikia vibaya kutokana na
hali aliyokuwa nayo mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa
akiishi na mama yake aitwaye Mariana, 36.
Aliacha shule huku marafiki zake wengi
wakimtenga kutokana na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu
kutokana na hali yake.
'Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.'
Miezi michache baadae alifanikiwa kupata
boyfriend, Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya
kusikia stori yake.
Sasa, miaka minne baada yote kuanza, madaktari wa wamefanikiwa kutatua tatizo lake.
No comments:
Post a Comment