Njemba moja wa mjini alitumiwa meseji na rafiki yake wa kiume ambaye
kwa bahati mbaya hakuhifadhi namba yake ya simu yake kwenye simkadi
yake. Kutokana na urefu wa meseji ikashindwa kuonekana yote mwishoni
ikaandika
‘some text missing…’
kwa vile jamaa kimombo hakishuki hivyo maneno ya mwisho hakuelewa
maana yake lakini akahisi litakuwa neno la kimapenzi miss you kutoka kwa
mchumba wake
Ili naye aonekane mjanja na anakijua kimombo akajibu hivi,
“some text missing too dear”
Kumbe ile message ilitoka kwa rafiki yake wa kiume
Jamaa ilibidi acheke tuu kwa sababu ya majibu ya swahiba wake
No comments:
Post a Comment