Kuna
mambo kadhaa ambayo msichana anatakiwa kuwa makini nayo katika
kuhakikisha uchumba wake unadumu na kufikia hatua ya kuolewa na kwenda
kuanza maisha mapya.
Yapo mengi lakini nitagusia matano ambayo kwa utafiti wangu ndiyo
Mazoea na wanaume
Wapo ambao wamejikuta wakiachwa solemba kufuatia tabia zao za kuwa na mazoea ya kijinga na wanaume.
Yawezekana
kabla ya kuchumbiwa marafiki zako wakubwa walikuwa wanaume (Wapo
wanawake wa aina hiyo). Unachotakiwa kufahamu ni kwamba hakuna mwanaume
anayefurahia ukaribu wa mchumba wake kwa wanaume wengine.
Hata kama
hakuna uhusiano wa kimapenzi lakini epuka sana kujichekelesha kwao,
kuongozana nao, kukaa nao au hata kuwasiliana nao. Ukifanya hivyo
utakuwa unamkwaza mchumba wako na inaweza kuwa moja ya sababu za
kukuchenga.
Marafiki micharuko
Ukishachumbiwa,
kuna marafiki zako ambao ‘automatikale’ unatakiwa kuachana nao.
Nazungumzia wale micharuko ambao hawawezi kukushauri vizuri juu ya
maisha yako.
Hata wale ambao wamekuwa wakikushawishi kila wikiendi
muende mkajirushe, baada ya kuchumbiwa unatakiwa kujiweka mbali nao ili
kumpa amani mchumba wako.
Tabia za kisichana
Ukishachumbiwa
wewe si msichana tena, utakuwa ni mama mtarajiwa wa familia yako. Tabia
za kisichana kama vile kuvaa mavazi yasiyo ya heshima, kukaa vijiweni
kuongea mambo ya umbeya na nyinginezo kama hizo hutakiwi kuendelea kuwa
nazo.
Kujifanyisha
Alichokupendea
huyo mchumba wako anakijua mwenyewe, kwa maana hiyo unatakiwa kuendelea
kubaki wewe kama wewe. Usijifanyishe kwa namna yoyote kama ambavyo
baadhi ya wasichana wamekuwa wakifanya.
Eti umeshaolewa
Kuolewa
ni mpaka pale mtakapoingia kanisani, msikitini nk na kufungishwa ndoa.
Kama bado hamjafika huko, wewe bado ni mchumba tu na hata kwenye ndoa
unaweza usifike.
Kwa maana hiyo hutakiwi kuhamia kwa mwanaume kama
ambavyo baadhi wamekuwa wakifanya. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba
kitendo cha wewe kuchumbiwa kisha kuamua kubeba virago vyako na kwenda
kuishi na mwanaume ni kuwakosea wazazi.
Msomaji wangu, yapo mengi ya kuepuka mara tu unapochumbiwa lakini haya machache yanatosha kwa leo. Jiangalie tabia zako, zile ambazo unajua wanaume wengi haziwafurahishi, jiepushe nazo ili kumjengea mchumba wako mazingira ya kukamilisha taratibu za ndoa yenu.
No comments:
Post a Comment