Mbunge
wa Arusha Mjini mheshimiwa Godbless Lema jana alizua gumzo kwa
wapiga kura wake baada ya kuamua kuzigawa picha za kutengeneza
zilizokuwa zikisambazwa katika mitandao ya Kijamii zikimuonyesha
akilawitiwa.
Muda
mfupi baada ya mkutano huo kuanza, Lema alimuita Mke wake (Neema)
na kumtaka azigawe picha hizo kwa wananchi ambazo alikuwa
ameziprint kwa wingi..
Wananchi
waliokuwa kwenye mkutano huo walikataa kupewa picha hizo na kusema
kuwa hazina umuhimu wowote kwao na wakamtaka mbunge huyo
azichome moto kwa kuwa wanajua ni za kutengeneza .
Baada
ya mabishano ya dakika kadhaa, Godbless Lema aliamuru kura zipigwe
kati ya wanaosema wapewe na wanaotaka zichomwe moto .Waliosema
picha zichomwe moto walishinda.
Baada
ya kura hizo, picha zilichomwa moto na Lema akawashukuru wapiga
kura wake kwa kuonyesha heshima kwake kwa kuzikataa picha hizo...
No comments:
Post a Comment