WAZIRI MKUU WA UKRAINE JULIA TYMOSHENKO AANZA MGOMO WA KUTOKULA CHAKULA NCHINI HUMO.
Waziri Mkuu wa zamani wa Ukraine, Julia Tymoshenko. |
Tymoshenko,
kiongozi mwenza wa muungano uliofanya mapinduzi yaliyopewa jina la
chungwa, mwaka 2004, unaounga mkono mataifa ya Magharibi, alitangaza
kuanza mgomo huo katika barua yake aliyowaandikia wafuasi wapatao 20,000
jana Jumatatu wanaounga mkono mkataba wa ushirikiano
kati ya Ukraine na Umoja wa Ulaya, ambao wanaandamana mjini Kiev kwa siku ya pili mfululizo.
kati ya Ukraine na Umoja wa Ulaya, ambao wanaandamana mjini Kiev kwa siku ya pili mfululizo.
Tymoshenko
aliyekuwa waziri mkuu wa Ukraine, amesema ataendelea kugoma hadi hapo
Rais Viktor Yanukovych atakaposaini mkataba huo kuhusu ushirikiano na
biashara huru na Umoja wa Ulaya.
Ameongeza
kusema kuwa iwapo Yanukovych hatosaini mkataba huo tarehe 29 ya mwezi
huu wa Novemba, atolewe katika uongozi wa Ukraine kwa njia ya amani na
kikatiba, pamoja na wasaidizi wake wa kisiasa na wala rushwa.
Polisi wakipambana na waandamanaji mjini Kiev. |
Taifa
hilo la watu milioni 45, linajikuta katika mzozo mpya wa kisiasa
uliosababishwa na uamuzi wa ghafla wa serikali wa kuubatilisha mkataba
wa kihistoria na Umoja wa Ulaya katika mkutano wake utakaofanyika
Vilnius, mji mkuu wa Lithuania baadaye wiki hii.
Uamuzi
huo umepitishwa baada ya Yanukovych kufanya mazungumzo ya siri na Rais
wa Urusi, Vladmir Putin mjini Moscow. Mazungumzo hayo yalikuwa
yanasadikiwa kuelezea vikwazo vikali ambavyo Urusi ingeviweka dhidi ya
Ukraine, iwapo ingeusaini mkataba huo na Umoja wa Ulaya.
Mkataba huo unaiweka wapi Ukraine?
Mkataba
huo wa ushirikiano ungeiweka Ukraine katika nafasi nzuri ya kuwa
mwanachama wa Umoja wa Ulaya hapo baadaye na kuiondoa nchi hiyo kuwa
mhimili wa kihistoria wa Urusi.
Hata
hivyo, Rais Putin anaiona Ukraine kama mwanachama muhimu mpinzani wa
kiuchumi katika umoja unaojulikana kama Umoja wa Forodha wa nchi za
Ulaya na Asia, ambao tayari unazijumuisha Kazakhstan na Belarus.
Jana
jioni, Rais Yanukovych aliwataka wananchi wake kuwa watulivu na
kuutetea uamuzi huo kwamba ulizingatia hatari za kiuchumi ambazo nchi
hiyo ingezipata iwapo ingevuja uhusiano wake wa kibiashara na Urusi.
Rais Viktor Yanukovych na Rais Vladmir Putin. |
Uamuzi
huo umetolewa baada ya bunge kushindwa kwa mara nyingine kuupitisha
muswada wa sheria utakaoruhusu kuachiwa huru kwa Tymoshenko, sharti kuu
lililotolewa na Umoja wa Ulaya ili nchi hiyo iweze kusaini mkataba huo.
Tymoshenko anatumikia kifungo cha miaka saba gerezani baada ya
kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.
Jana
Jumatatu, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatanya zaidi ya
waandamanaji 100,000 wanaoupinga uamuzi huo wa serikali waliokusanyika
mjini Kiev.
Umati
huo wa watu unaelezwa kuwa mkubwa zaidi kutokea tangu mapinduzi ya
chungwa na baadae Viktor Yushchenko kutoka muungano unaounga mkono
mataifa ya Magharibi, kushinda katika uchaguzi wa urais mwaka 2007.
Source->DW
No comments:
Post a Comment