MTAYARISHAJI mahiri wa muziki wa
Kizazi kipya, anayemiliki studio za ya B Hits, Hermes Bariki ‘Hermy B’
ameteuliwa kuwa Jaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba Afrika
Mashariki la Tusker Project Fame.
Mkali huyo anayemiliki studio za B
Hits, ataiwakilisha Tanzania na kwa kuungana na majaji wengine jijini
Nairobi, nchini Kenya akichukua nafasi ya Zahir Zorro aliyekuwa Jaji
katika shughuli ya kusimamia usaili wa shindano hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Tusker, Sialouise Shayo, alisema
katika kuelekea awamu ya kwanza ya shindano hilo msimu huu wa sita,
wamejipanga kuhakikisha Watanzania wanahusishwa kikamilifu.
“Kama tunavyomkaribisha Jaji mpya
Hermy B ambaye amekuwa katika kinyang’nyiro hiki cha Tusker Project Fame
kwa muda mrefu, tunatumia fursa hii kuwatangazia Watanzania kuwa
tumejifunza mengi kupitia kwa Zorro,” alisema.
Katika shindano hilo, Tanzania inawakilishwa na Angela Karashani, Elisha Simon, Mgeni Kalinga na Ussa Dubart.
Kwa upande wake, Hermy B aliishukuru Tusker kwa kumchagua kuwa Jaji katika shindano hilo kwa mara ya sita pamoja na Zahir Zorro.
Mshindi wa Tusker Project Fame atajinyakulia Sh 100, 000, 000 na mkataba wa kurekodi utakaogharimu Sh 200, 000, 000.
-Mtanzania
No comments:
Post a Comment