TTCL

EQUITY

Monday, August 5, 2013

Lema aing’ng’ania polisi bomu la Soweto Arusha

Mbunge wa Arusha, Godbless Lema 


Arusha. Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, ameendelea kushikilia madai yake kuwa polisi wanahusika na tukio la bomu lililolipuka  katika mkutano wa kampeni ya chama hicho Viwanja vya Soweto  Arusha na kusababisha vifo vya watu wanne.
Lema alitoa madai hayo juzi alipohutubia mkutano wahadhara Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.
Alidai Rais Jakaya Kikwete amegoma kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo, ili kunusuru  polisi na aibu ya kushiriki uhalifu na mauaji ya raia wasio na hatia.
“Mauaji ya Soweto yalipangwa na kutekelezwa na  polisi, RPC (Kamanda wa Polisi) wa Arusha anajua mpango mzima ndiyo maana Rais hataki kuunda tume kama Chadema tulivyomuomba, ili tuwasilishe ushahidi wa video kuonyesha jinsi walivyohusika,” alisema Lema
Alisema ushindi wa Chadema kata nne za Elerai, Kimandolu, Themi na Kaloleni ni dalili njema za ushindi kwa nafasi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Naye Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alitaka polisi kukitambua na kukiheshimu Chadema na viongozi wake,  kwa sababu ni chama kilichoundwa na kuongozwa kwa kuzingatia katiba na sheria za nchi.
“Hatutakubali kuonewa, kunyanyaswa wala kupuuzwa kwa sababu iwayo yote,” alisema Golugwa.
Alishukuru  ulinzi wa Mungu mlipuko wa bomu, ushindi na walitangaza kuanza vikao vya  katiba leo.

No comments:

Post a Comment