Fred Nyman - mwanzilishi wa RHM
Historia ya Redio Habari Maalum
RHM (Redio Habari Maalum) kwa sasa Habari
Maalum media. Ni studio inayoshughulika na uandaaji wa vipindi vya
Redio ambavyo vinarekodiwa na kurushwa katika Stesheni
mbalimbali. Habari Maalum Media iko kilometa kumi na tano (15km)
Kaskazini mwa mji wa Arusha barabara iendayo Nairobi kupitia Namanga.
Mwanzilishi wa kazi hii ni Mchungaji Fred Nyman kutoka Finland. Lengo
kuu la kuanzishwa kwa Redio Habari Maalum ni kuwafikia watu kwa injili,
wapatao milioni 70 wanaozungumza kiswahili katika eneo la Afrika
mashariki na kati. Maandalizi ya kipindi cha kwanza yalianza kwenye
miaka ya sitini. Tarehe 05/09/1976, kipindi cha kwanza cha dakika kumi
na tano kilirushwa na FEBA Radio huko Seychelles kupitia masafa mafupi
au short wave (SW) na mtangazaji wa kwanza aliyetangaza kipindi hicho
alikuwa Mchungaji Fred Nyman wa Finland ambaye kwa sasa ni mchungaji
nchini Finland.
No comments:
Post a Comment