Kama nchi, Tanzania imesaidiwa kwa kiasi kikubwa na Marekani kupitia miradi mbalimbali
Dar es Salaam.
Watanzania wanasubiri kwa hamu ujio wa Rais Barrack Obama kuwa utakuwa ni neema katika harakati za kujiletea maendeleo.
Watanzania wanasubiri kwa hamu ujio wa Rais Barrack Obama kuwa utakuwa ni neema katika harakati za kujiletea maendeleo.
Ni heshima kubwa kama taifa kupokea ugeni mzito wa kiongozi wa dola lenye nguvu zaidi duniani.
Kumbuka mwezi Machi Tanzania ilipokea ugeni wa
Rais Xi Jinping wa China, ambayo katika siku za karibuni imekuwa na
nguvu za kutisha katika medani ya uchumi duniani.
China ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania,
lakini katika miaka ya karibuni Marekani imetoa fedha nyingi za misaada
na kuanzisha miradi mikubwa ya kuisaidia Tanzania.
Marekani ni kati ya washirika wakubwa wa maendeleo
kwa Tanzania kwani katika mwaka 2012 ilimwaga misaada yenye thamani
ya Dola750 milioni (Sh1.2 trilioni) kusaidia shughuli za maendeleo.
Nchi hiyo kupitia mfuko wa Global Fund imekuwa ikigharamia kampeni za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.
Global Fund inafanya kazi kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Umoja wa Mataifa (UN).
Pia, kuna miradi mbalimbali ya kilimo cha
umwagiliaji, elimu, ulinzi na masuala ya ushauri katika usimamizi wa
fedha. Shirika la Maendeleo la Marekani (Usaid) lilitoa Dola 350
milioni (Sh558 bilioni) kwa mwaka 2012 kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia, limemwaga kiasi kingine cha Dola10.5 milioni
(Sh16 bilioni) kwa ajili ya ujenzi wa sehemu za kuhifadhia dawa kwa
Tanzania Bara na Zanzibar.
Usaid, pia imekuwa ikisaidia katika harakati za
kuinua uelewa wa kinamama katika kutambua haki zao. Tayari, watu wapatao
23,000 wamenufaika kutokana na mpango huo.
Katika kipindi cha miaka mitano, shirika hili limetoa kiasi cha
Dola 698 (Sh1.1 trilioni) ili kusaidia katika kuimarisha sekta za
usafiri, nishati na maji.
Pia, Serikali ya Marekani imekuwa ikisaidia katika
kuka-mbana na rushwa na hasa katika masuala ya manunuzi. Pia imekuwa
ikitoa misaada mingi kwa Taasisi ya Kupambana na Kukabiliwa na Rushwa
(Takukuru).
Mradi wa Feed the Future (FTF)
Serikali ya Marekani inaunga mkono Programu ya
Tanzania ya kuinua kilimo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ili
kujenga uwezo wa kujitosheleza kwa chakula.
Inagharamia mpango huo kupitia mradi wa Feed the Future, ambao unafadhiliwa na ofisi ya Rais wa Marekani.
Asilimia 80 ya fedha za taasisi hiyo zinagharamia
mpango wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).
Mpango huo una lengo wa kupandisha kilimo katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya,
Iringa na Rukwa.
Mpango wa Partnership for Growth
Rais Barrack Obama ameanzisha mpango wenye jina la
`Partnership for Growth’ wenye lengo la kukabiliana na changamoto
zinazokwamisha uchumi wa Tanzania kukua. Changamoto hizo kama zime za
umeme na matatizo ya miundo mbinu.
Mradi wa PEPFAR
Mradi unaoitwa President’s Global Health
Initiative (PEPFAR) unaendesha kampeni kubwa ya kukabiliana na ugonjwa
wa Ukimwi. Tangu mwaka 2004, Tanzania imepokea Dola2.2 bilioni (Sh3.5
trilioni) kutoka taasisi hii.
Pia, inaunga mkono kampeni ya kuhamasisha watu kupima ili kufahamu kama wana ugonjwa wa Ukimwi.
Mpango huu unasimamiwa na Serikali ya Marekani na ndio kwa kiasi
kikubwa unasaidia kampeni ya kukabiliana ugonjwa wa Malaria nchini
Tanzania. Mradi huu umesaidia kusambaza vyandaruai milioni sita kwa
wanawake na watoto. Kampeni hii imesaidia kushusha maambukizi ya malaria
kwa asilimia 45 kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano.
Peace Corps
Serikali ya Marekani imekuwa ikileta wafanyakazi
wa kujitolea hasa katika sekta ya elimu tangu mwaka 1962. Wafanyakazi
hao kupitia mpango unaoitwa Peace Corps Volunteers. Wafanyakazi hao wa
kujitolea huja kwa ajili ya kusaidia katika sekta za elimu na afya.
Walimu wa wanaokuja nchini huwa zaidi wa maomo ya sayansi na hisabati.
Wakati wengine husaidia sekta ya afya.
Ushirikiano wa sekta ya Ulinzi
Wanajeshi wa Marekani hutumwa nchini kufanya kazi za kujitolea kama zile za kuchimba visima, kujenga shule na zahanati.
Pia , nchi hiyo hutoa mafunzo kwa majeshi ya
Tanzania ili wafanye kazi kwa ufansi kwenye kazi za kulinda amani.
Tanzania hivi sasa ina majeshi katika nchi za Lebanon, Sudan na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Halikadhalika. Wamarekani hufundisha wanajeshi na
polisi wa Tanzania. Kuanzia askalit 15-20 hupata mafunzo kila mwaka
nchini Marekani.
Benki Kuu ya Tanzania
Marekani imeweka mtaalamu wake katika Wizara ya
Fedha ili kushauri namna nzuri ya ulipaji madeni ya Tanzania. Mtaalamu
huyo anfanya kazi na Wizara na Benki Kuu (BoT).
Kubadilishana uzoefu
Pia, Watanzania wapatao 20 kila mwaka huwa
wananufaika na Marekani katika mpango wa kubadilishana wanafunzi na
wataalamu. Mpango huu umenufaisha watu kutoka Bara na Zanzibar.
Wanafunzi na wasanii wa Tanzania wamepata nafasi ya kuzuru Marekani
kushiriki katika matamasha mbalimbali huko.
Pia, kuna mifuko mbalimbali, ambayo inasaidia maendeleo ya
Watanzania kama ule wa Mfuko wa Balozi wa Marekani wa Kulinda vivutio
vya Utamaduni, pia kuna Mfuko wa Kukabiliana na tatizo la Uhamiaji
Haramu na mwingine kwa ajili ya kushughulikia masuala ya demokarisa Haki
za Binadamu.
Mifuko yote imetoa mamilioni ya fedha, ambayo Watanzania wamenufaika nayo.
No comments:
Post a Comment