TTCL

EQUITY

Wednesday, June 26, 2013

UJIO WA OBAMA

 "MAMA WATOTO BAKI HAPA UNISONGEE UGALI TAFADHALI!!!."

Tayari zimeshaandaliwa Kanga,Vitenge na Viremba kwa wake zetu kuvaa sura ya Kidume wa Dunia,
Eti kwamba Mke wangu aache kunitengenezea ugali mtamu wa Dagaa,bamia na nyanya chungu ili aende akapange mstari Kandokando mwa barabara akipaushwa na jua la darisalama kwa kuimba na kumpokea Obama!,

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema"Unaweza kupewa chembe za chupa ukambiwa ni almasi halafu ukaenda unashangilia kama zuzu........."
tunaangalia mantiki iliyopo ya ujio wa watu 700 ni tishio.
wote wakiandamana na Rais Obama,Tunashangilia na kuandaa mapokezi eti tutafaidika,
tumesahau ya kwamba tumezidiwa utashi na kwamba tujiandae kwa vita ya utashi kuliko kuandaa mahoteli na usafiri!.
Mabilioni yatatumika kuandaa ma-tshirt,Kanga,vitenge,malazi,mafuta n.k.yaani mabiloni ambayo nchi masikini ingetakiwa ijenge mashule,iongeze mishahara ya walimu,ichimbe visima n.k

Walalahoi ambao wengi ni machinga wametimuliwa wote maeneo ya mjini wasionekane na hivyo wakome na njaa mpaka bosi aondoke.

Abiria wanaoingia Dar kutoka mikoani kwa sasa wanakosa amani maana ukaguzi wa Satellite mpaka kwenye unyayo!

### NINI MAONI YAKO KUHUSU ZIARA HII??!!.

No comments:

Post a Comment