WAKILI WA HENRY KILEO NA JOYCE KIRIA AFUNGUKA.
Henry na Joyce siku yao ya ndoa
RE: HENRY JOHN KILEO.
BAADA YA SINTOFAHAMU KUHUSU
KILICHOMSIBU HASA HENRY JOHN KILEO, NA BAADA YA MAJIBU YA JESHI LA
POLISI KUHUSU JUHUDI ZA JOYCE KIRIA KILEWO KUFAHAMISHWA ALIKO MUMEWE
HENRY JOHN KILEWO, NA BAADA YA MASWALI MENGI KWANGU KAMA WAKILI WA
KILEWO NA KIRIA, NIMEONA YAFAA NITOE MAELEZO HAYA KWA KIREFU.
Henry John Kileo alipigiwa simu na
Maafisa wa Polisi Makao Makuu mnamo Tarehe 17/6/2013, wakimuarifu kwamba
wanataka kufanya mahojiano naye.Hawakusema ni kuhusu nini.mara moja
Kilewo akawasiliana nami kama wakili wa familia yao na Joyce Kiria,nami
nikawasiliana na maafisa hao kuwaarifu kwamba kwa kuwa nina majukumu
kadhaa ya kkimahakama, na kwa kuwa Kilewo yuko nje ya mkoa,basi
ninaahidi kama wakili kuhakikisha ninamepeleka binafsi Kilewo Makao
Makuu Police mnamo Ijumaa ya tarehe 21/6/2013.
Tarehe 21/6/2013 tuliambatana mimi,
Kilewo na John Mnyika (MB) mpaka Police Makao Makuu, ambapo Mnyika
alituacha na Kilewo;mahojiano yakaanza.Kwa ujumla walimuhoji Kilewo
mambo mbalimbali kuhusiana na tukio la kumwagiwa tindikali kijana
aitwaye Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mnamo mwaka
2011.Wakati mahijiano hayo yanafanyika,tayari kulikuwa na Case ya jinai
ikiendelea huko Igunga, ambapo washtakiwa Wanne (4) ambao ni makada wa
Chadema kutoka maeneo mbalimbali nchini walishtakiwa kama mshtakiwa
nambari moja mpaka nne.Walishtakiwa kuhusiana na tukio hilo
nililolisema, la Mussa Tesha kumwagiwa Tindikali.Walishtakiwa chini ya
vifungu vya sheria ya kanuni ya adhabu, (Penal Code, na si ugaidi).
Baada ya mahojiano na Police
yaliyomalizika kwa Kileo kuandikisha statement mpaka mnamo saa 11.30
hivi za jioni ya hiyo Tarehe 21/6/2013, Police walimnyima Kilewo
dhamana, na wakampeleka remand iliyoko Central Police Station,akalala
huko.
Jumamosi ya mnamo tarehe 22/6/2013,
mimi wakili, Joyce Kiria na John Mnyika tulifika Central Police station,
ambapo OCS wa hiyo Central Police Station alituarifu kwamba amri
alizonazo ni kwamba Kilewo haruhusiwi kuonana na mtu yeyote. Kama wakili
nilijadiliana masuala ya kisheria na OCS, ikalazimu kuwasiliana na
maafisa wa Police Makao Makuu ambao hatimaye waliniruhusu mimi kama
wakili kwa mujibu wa sheria kuonana na mteja wangu.
Tukazungumza na kupeana "moyo",
nikahakikisha amekula chakula kilicoletwa na mkewe Joyce Kiria (ambaye
muda wote alikuwa akimuangalia mumewe kwa mbali tu,kwani mazungumzo
yangu na Kilewo yalifanyika faragha).
Mnamo saa 7.30 hivi tuliondoka sote
(wakili, Kiria na Mnyika), na kukubaliana kurudi tena Central Police
Station Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 kumtembelea tena Kilewo, na pia
kufahamu mipango hasa ya jeshi la Police kuhusu Kilewo kwani mpaka
tunaondoka si wakili wala mkewe Kilewo aliyefahamishwa rasmi kuhusu
mipango hiyo.
Nikiwa Nyumbani nilipokea simu toka
kwa Joyce Kiria akiniarifu kwamba amefika Central Police Station jioni
ya Jumamosi ya tarehe 22/6/2013 na kuarifiwa tu kwa mkato kwamba Henry
John Kilewo "ameondoka".
Ukweli kama mke alikuwa
amechanganyikiwa, na jukumu la kwanza lilikuwa kumtuliza kisaikoilojia
kwani nilifahamu kina Kilewo walikuwa wamepata mtoto muda si mrefu huko
nyuma;kwa hiyo hali ya Joyce ilikuwa delicate sana kiafya na
kisaikolojia.
Nikapambana kama wakili kwa kutumia uzoefu na contacts (P.R) ili kupata tarifa ya aliko mteja wangu.
Niliariwa tu "off record" na maafisa
wa Police kwamba Kilewo amesafrishwa kwa ndege ya Precision kuelekea
Tabora kupitia Mwanza chini ya ulinzi wa maafisa Senior wa Police ili
kule Tabora afunguliwe Case.Sikuwa na mawasiliano yeyote na mteja wangu,
na hizo taarifa "off record" ndo cha pekee tulichokuwa nacho mimi,
Joyce Kiria na uongozi wa Chadema kuhusu nini kimemsibu Henry Kileo.
Niliendelea kupambana kupata taarifa
rasmi, na hatimaye Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 majira ya saa 6 hivi
(noon) ndipo nilipopigiwa simu na mmoja wa maafisa waliomsindikiza
Kilewo kuelekea huko Tabora kwa utaratibu ule ule wa "off record", na
kuniunganisha na Kilewo, ambapo nilizungumza naye kwa kifupi kumjulia
hali na kumuhakikishia kwamba tutapigana kwa uwakili wetu wote kwa ajili
yake.
Kwa hiyo mpaka muda huo hatukuwa bado
na uhakika wa 100% kwamba Kilewo yuko wapi hasa. Kw wale mawakili
wenzangu wanafahamu kwamba huwezi tegemea taarifa za kusikilizishwa
mteja kwenye simu ambayo hata si ya kwake.Wala huo si ushahidi wa alipo
mtu huyo kisheria.
Lakini ikatubidi ku-"assume" kwamba
Kilewo yuko/atapelekwa Tabora kushtakiwa.mimi na Prof Abdallah Safari
tukaanza maandalizi ya upesi upesi ya safari kuelekea Tabora kwa gari
(kwani ndege kuulekea Tabora ni Jumamosi na Jumatatu tu). Tuliondoka kwa
gari ya makao makuu ya Chadema Jumapili ya tarehe 23/6/2013, majira ya
saa 11.30 hivi za jioni. Tulisafiri usiku kucha, na tulichukuwa "risk"
ambazo kwa kawaida tusingechukuwa, ikiwemo kupita katika mapori maarufu
kwa utakaji;kilichotusukuma na kutupa moyo ni kwamba Henry John Kilewo
yuko mahali ambapo anatuhitaji sana, na hana tumaini lingine bali sisi
mawakili wake.
Tukisafiri usuku kucha na kufika
Tabora asubuhi ya Jumatatu tarehe 24/6/2013, majira ya saa 2.30
asubuhi;tumechoka hakuna mfano.Tukabadili mavazi upesi upesi na kuvaa
suits zetu na kukimbilia mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, ambapo
turiarifiwa kuwa wao hawana taarifa zozote za Kilewo. Tukaelekea Makao
Makua ya Police Tabora;jibe likawa ni lile.
Maana yake ni kwamba sisi mawakili wa
Kilewo, tuko Tabora ambayo ni kubwa has, na hatujui mteja yuko wapi
hasa. Nikafanya juhudi zile zile za "off record", na kufahamishwa kwamba
Kilewo alishikiliwa Police Station ya Nzega (masaa matatu toka Tabora),
na kwamba yuko njiani kuletwa Tabora.Hatukuwa na uhakika bado, ila
ilitulazimu kushikilia hako kataarifa kasiko rasmi, na kuendelea na
maandalizi ya case.
Majira ya saa 9 hivi za alasiri ya
Tarehe 23/6/2013 Kilewo, akiwa chini ya ulinzi mkali sana wa FFU katika
Land Cruisers Mbili za Police waliwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi
Tabora; hajala tangu jana yake.
Alikuwa yeye na wenzake wanne ambao
walikuwa wamefutiwa mashtaka kwa hati ya "Nolle Prosequi" huko Igunga,
kisha kukamatwa tena mara moja na kusafirishwa kwa ulinzi mkali sana
mpaka Tabora.
Ukweli ni kwamba tulivyoonana na
Kilewo si mawakili wala KIlewo mwenyewe aliyejizuia kulengwa na
machozi;yeye akimshukuru MUNGU kwamba tumepambana na yote mpaka Tabaora
kwa ajili yake kwa kasi vile, nasi kwamba hatimaye tumeonana na mteja
wetu.
Tukaingia Mahakamani, Kilewo na
wenzake wakasomewa mashtaka mawili; moja chini ya sheria ya kuzuia
ugaidi kwamba walimteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga,
Tabora na la pili kwamba walimdhuru kwa kumwagia Tindikali.
Makosa ya Ugaidi hayana dhamana.
Mawakili tulipambana na kutoa hoja za
kisheria nne (4) dhidi ya uhalali wa mashtaka yenyewe na utaratibu wa
kufungua case husika. Tumeoimba mahakama kufuta mashtaka ya ugaidi, au
la iamuru kila mshtakiwa arudishwe kushtakiwa mahali alikokamatwa (mfano
Kilewo, Dar es Salaam).
Uamuzi wa Mahakama ni tarehe 8/7/2013.
Kabla ya kuondoka Tabora jana,
tulipita kumuaga Henry Kilewo na wenzake katika gereza la Uyui. Wote
wako na combat zao za chama chao, na wako imara, hasa baada ya kuona
mawakili wako imara.
Cha msingi ni kuomba MUNGU aipe mahakama ujasiri.
Peter Kibatala, Advocate.
No comments:
Post a Comment