Walichotofautiana Shekhe Kitilla na RPC Dodoma;Hiki hapa!
Kamanda wa Polisi (RPC) wa Mkoa wa Dodoma, David Misime (katikati), alipokuwa na kikao na Viongozi wa
Madhebu ya Dini ya Ki-Islamu na Wakristo aliowaita Ofisini kwake kwa Mazungumzo
ya Mahusiano Mema ili kukomesha
Ajali, Mauaji, na Vitendo Viovu mkoani
humo.
Na Bryceson Mathias
‘Mshale kwenda Msituni haukupotea!’
INGAWA
waswahili husema, “Mshale kwenda msituni haukupotea”, hivi karibuni
Usemi huo ulibadilika, ambapo Shekhe wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani
Said Kitilla, alitofautiana kimtazamo na Mkuu wa Polisi (RPC), David
Misime.
Shekhe
Kitilla alitofautiana kimtazamo na Mesime katika kikao cha mahusiano ya
ujirani mwema, ambapo Polisi iliwaangukia Viongozi wa Dini ikiwaomba
washirikiana kubaini Uhalifu na Wahalifu, ambao wengi ni Waumini wao.
Nia
ya Misime kwa viongozi wa Dini aliwaita kuwataka wajenga mahusiano ya
pande hizo mbili (Polisi na Viongozi wa Dini), ili katika mahubiri yao
wawaonye waumini wao, kuachana na vitendo viovu vinavyosababisha Maafa
na Vifo mkoani.
Alivitaja
Vitendo viovu vinavyosababisha Maafa na vifo kuwa ni pamoja na
Kuendesha Bodaboda na Magari Kasi, Utumiaji wa Vilevi, Madawa, Ngono
Zembe, Ukahaba na Mambo yanayofanana na hayo.
Ilieleza
Vitendo hivyo vinasababisha Vifo, Ulemavu, Wizi, Ujambazi na Uharibifu
wa Mali na Maisha ya watu, jambo ambalo alidai, Viongozi hao wa Kidini
wakitumia Doria yao ya Kiroho, na Polisi wakatumia Doria yao ya
Kimwili,Amani na Usalama nchini vitakuwepo, na uharifu utapungua.
Misime
aliwataka Viongozi wa Dini waendelea kuhubiri Utii wa sheria bila
shuruti, kutokana na wao kuwa karibu na wananchi kwa kuwa watu wakiitii
sheria hiyo, hata ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe wa
uovu huo, zitapugua.
“Mimi
ninawaheshimu viongozi wa dini kwa kuwa mnachangia utulivu na Amani
nchini, na hata mkiniona na kosa, msisisite kunionya kama mlivyofanya
zamani bila kuongopa cheo cha mtu”alisema Misime.
Misime
aliwaonya baadhi ya askari Polisi wasio waamnifu wanaovujisha siri
ambazo wananchi wametoa kuhusu uharifu na waharifu na kudai, ili
kudhibiti tabia hiyo askari watakaobainika watachukuliwa hatua za
kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Mchungaji
Kanisa la Moroviani Iringa Road, Kaminyoge Andendekisye, alisema
mahusiano kati ya Jeshi hilo na viongozi wa Dini, yalikuwa mabovu
kutokana na kutotambuliwa na kupuuzwa kama hawana uwezo wa kuleka hali
ya utulivu katika Jamii.
Ustadhi
Musa Juma alisema, kukaa na Polisi kunafanya watambuane na kufanikisha
utendaji wa kazi na kuuweka mji mfano wa Utulifu na Amani, lakini
ukafuatiwa na Mbunge Machali NCCR-Mageuzi kuvamiwa na Majambazi.
Viongozi
wa Ki-Islam na Kikristo waliahidi kutoa ushirikiano wa kuhubiri ombila
la RPC kwa waumini wao, lakini Shekhe Kitilla alitofautiana na wenzake
akidai Serikali ndiyo inaendekeza uharifu na Uovu ulioshamiri nchini.
Kitilla
alinukuu Mbinu alizotaja aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Tabora, Morogoro na
Mlezi wa Klabu ya Wandishi Morogoro (Moro Press Club), Stephen
Mashishanga, kuzuia Askari kutumia Nguvu wanapofautiana na Wananchi,
alipohojiwa na TBC1 karibuni.
Kitilla
alisema,“Viongozi wa Dini tukikemea Pombe, Serikali inatoa Vibali vya
Ulevi Baa, Viosk, zinazonywewa toka asubuhi na Kazi hazifanyiki.
Tukizuia Kondom, Serikali inaruhusu, Tukikemea Mavazi yasiyo na heshima,
Serikali iko kimya!
“Tukikemea
Michezo Michafu ya TV, Mavazi Nusu Uchi hasa Urembo na Miziki, Serikali
inatoa Ruksa, Tukikataza Ulevi, Sigara Serikali inaanzisha Viwanda
vyake.
No comments:
Post a Comment