John Mnyika (MP) |
Na Mwanablog
Pamoja
na kuwa wana ushahidi wa Picha, Mikanda ya Video inayoonyesha jinsi
Polisi walivyoshiriki kulipua bomu la Arusha, Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema wamesema hawapo tayari kupokea pesa zilizotengwa na
serikali kwa ajili ya mtu atakayetoa taarifa kuhusu waliohusika na
mlipuko wa Arusha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Ofisi za Chama hicho Makao Makuu, Msemaji wa
Chama hicho John Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo alisema “hata
kama bado hatujakaa kama Chama kuafikiana suala hili, hizo pesa
kuzichukua ni ufisadi tu, matumizi mabaya ya pesa, serikali imepata wapi
pesa za kulipa milioni mia kwa watoa taarifa wakati haijawahi hata
kutoa rambirambi kwa mjane wa Daudi Mwangosi, licha ya kwamba Polisi
walihusika kwa asilimia zote katika kuua, hatuwezi kuhuchukua hizo pesa.
Kwanza
ifahamike kwamba serikali imeamua kutenga hilo fungu ili kuhalalisha
matumi mabovu ili kuhalalisha ulaji wa pesa, ije iseme tuliwalipa watoa
taarifa, huu ni uongo, na serikali inapokuwa inadanganya raia wake
inakosa uadilifu wa kuendelea kutawala.
Suala
la Arusha ni tete, serikali imekuwa ikisema uongo hapa na pale, ndio
maana hata Mizengo Pinda tangu aseme uongo suala hilo halijawahi
kuzungumzwa Bungeni, Spika analipiga danadana kila mara.
Aidha
katika mkutano huo, Mnyika amelitaka jeshi la polisi liwaachie vijana
watatu wanaoteswa na Jeshi hilo ili kuwalazimisha kutoa mikanda
waliyorekodi ambayo Mbowe anasema wanayo inayoonyesha jinsi Polisi
walivyolipua bomu, kuwapiga risasi watu waliotaka kumkamata aliyelipua
bomu, na gari ya polisi iliyomtorosha mtu aliyerusha bomu. Jeshi la
Polisi mkoani Arusha linawashikilia vijana watatu makada wa Chadema, ili
liweze kupata mikanda hiyo kwa nguvu bila kutumia njia za kuwaomba.
No comments:
Post a Comment