TTCL

EQUITY

Tuesday, January 26, 2016

Waziri Lukuvi awaandikia wabunge wote barua.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh.William Lukuvi,amewaandikia wabunge wote barua akiwataka waeleze migogoro ya ardhi iliyopo katika majimbo yao.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Babati Mjini Cecilia Pareso (CHADEMA) aliyetaka kujua hatua za serikali katika kutatua migogoro ya ardhi baina ya wananchi wake na hifadhi ya mbuga za wanyama Tarangire.
''Mheshimiwa Spika mimi nimewaandikia wabunge wote barua na nikiwataka kila mmoja anieleze katika eneo lake mgogoro wa ardhi uliopo iwe ni kati ya vijiji na hifadhi ,misitu,au na wawekezaji ili iwe rahisi kwangu kuishughulikia''.Amesisitiza Lukuvi
Aidha Lukuvi ameongeza kuwa seRikali ya awamu ya tano imejipanga vyema katika kutatua kabisa matatizo ya migogoro ya mara kwa mara ya ardhi hapa nchini

No comments:

Post a Comment