TTCL

EQUITY

Friday, January 29, 2016

EU yaipa TANESCO Bil 96.7 kusambaza umeme.

Umoja wa Ulaya waipatia TANESCO shilingi bilioni 96.7 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma.
Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na nchi za Ujerumani na Ufaransa, zimelipatia Shirika la Umeme nchini TANESCO Euro Milioni 42, zaidi ya fedha za Tanzania shilingi bilioni 96.7, kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme katika mikoa ya Kaskazini Magharibi ya Geita, Kagera na Kigoma.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utolewaji wa fedha hizo, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, mhandisi Felchesmi Mramba, amesema fedha hizo zitawezesha ujenzi wa njia ya umeme yenye jumla ya kilomita 144 itakayounganisha mikoa hiyo kwenye gridi ya taifa.

Mbali ya fedha hizo, TANESCO pia imesaini mkataba mwingine na benki ya maendeleo ya nchini Ujerumani KfW ambapo taasisi hiyo ya nchini Ujerumani itaipatia msaada wa shilingi za Tanzania bilioni 17.7 kwa ajili ya miradi ya usambazaji umeme vijijini.

No comments:

Post a Comment