TTCL

EQUITY

Wednesday, December 30, 2015

Waziri Nape azindua Filamu ya Home Coming

2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihojiwa na  mtangazaji mashuhuri wa Azam TV Taji Liundi muda mfupi kabla ya kuzindua filamu mpya ya Home Coming kwenye ukumbi wa Century Cinema ,Mlimani  City jijini Dar es Salaam.

5
Wadau wa Sanaa na Utamaduni wakisubiri kushuhudia uzinduzi wa filamu mpya ya Home Coming.6
Mmoja wa washiriki wa Filamu hiyo ya Home Coming ,Susan Lewis maarufu kama Natasha
3

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihojiwa muda mfupi kabla ya kuzindua Cinema ya Home Coming.15
Muigizaji mkuu wa filamu ya Home Coming Daniel Kijo (kushoto) akisalimana na  mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo Waziri wa habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mara baada ya uzinduzi wa filamu hiyo  kufanyika kwenye ukumbi wa Century Cinema, Mlimani City jijini Dar es  Salaam.


KAMPUNI Alkemist Media inayojishughulisha na uandaaji wa filamu nchini,  usiku wa kuamkia leo ilizindua filamu mpya inayokwenda kwa jina la Homecoming.
Filamu hiyo iliyochezwa kwa mrengo wa kuelimisha juu ya masuala ya kutokomeza ufisadi mbalimbali, ilizinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,  ndani ya ukumbi wa kuonyeshea sinema uliopo katika jengo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza muda mfupi kabla ya uzinduzi huo kufanyika Nape alisema kuwa anawashukuru waandaaji wa filamu hiyo kwa kumpatia fursa ya pekee kwa ajili ya kuizindua filamu hiyo ikiwa ni moja ya mwendelezo wa kuthamini kazi za wasanii mbalimbali hapa nchini.
“Nimefarijika sana kuona leo tumekusanyika kwenye ukumbi huu kwa ajili ya kuzindua filamu ya Kitanzania, hivyo niwapongeze wamiliki wa ukumbi huu kwa kuruhusu kuonyeshwa kwa filamu hii hapa, najua ni mwanzo na itakuwa faraja zaidi siku nyingine nikija hapa nikute filamu  zetu zikionyeshwa maana najua huwa ni adimu mno kuona sehemu kama hii watu wameketi kuangalia filamu zetu..
“Kufanya hivi mimi nina imani kuwa ni njia mojawapo ya kukuza soko letu ambalo tunajitahidi kupambana ili tuweze kutokomeza wizi huku tukinyanyua ajira kwenye sanaa hii,” alisema Nape.

18 
…wakipiga picha ya pamoja na Mh. Nape NnauyeNape na homecoming (1)  Nape na homecoming (3) Nape na homecoming (4) Nape na homecoming (5) Nape na homecoming (6) Nape na homecoming (7)   Nape na homecoming (10)  Nape na homecoming (12)  Nape na homecoming (14)   Nape na homecoming (17)   Nape na homecoming (20) Nape na homecoming (21) Nape na homecoming (22) Nape na homecoming (23)
1716
 12
 Mzee Chilo’ na Daniel Kijo.
109

No comments:

Post a Comment