TTCL

EQUITY

Thursday, December 17, 2015

Rais Magufuli Awahakikishia Watanzania Kutimiza Ahadi Yake Ya Elimu Bure.......

Aipongeza TRA kukusanya Trilioni 1.3 Ndani Ya Mwezi Mmoja, Atoa ONYO kwa Wakuu Wa Mikoa

Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300.
Kutokana na mafanikio hayo makwa amewahakikishia watanzania kuwa fedha kwa ajili ya kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari ambazo ni kiasi cha shilingi Bilioni 131 zitatengwa mwezi huu na kupelekwa moja kwa moja katika shule husika.

Amesema wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa watapatiwa nakala za taarifa za ugawaji wa fedha hizo na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzitumia vibaya.

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa fedha hizo ambazo ni pamoja na fedha za maendeleo, fedha za mitihani na fedha vifaa vya kufundishia zitaanza kutumwa kila mwezi kuanzia mwezi huu wa kumi na mbili.

No comments:

Post a Comment