TTCL

EQUITY

Saturday, June 27, 2015

Watu watatu wafariki wawili kati yao wanasadikiwa ni magaidi wilayani Mvomero

Watu watatu wamefariki dunia  wawili kati yao  wanasaidikiwa  kuwa ni kundi la magaidi pamoja na raia mmoja baada mapigano kutokea kufuatia  msako uliofanywa na jeshi la polisi kwa kundi  la vijana wanaojinadi  kuwa ni magaidi wapato 50  waliokuwa na silaha mpakani mwa mkoa wa Tanga na Morogoro kupitia msitu wa mziha turiani wilayani Mvomero.

Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro(ACP) Mussa Marambo akizungumza na waandishi wa habari ofisi  kwake amesema jeshi la polisi mkoa wa Morogoro wakishirikiana na askari wa mkoa wa Tanga linawashikilia watu sita wanaojinadi kuwakundi la magaidi  kufutia msako mkali  uliofanyika baada kuona kundi la vijana  wasiojulikana watokako wakiwa na silaha mbalimbali za moto  wakielekea mkoani morogoro na wamekimbilia katika misitu.

Kwamujibu wa matroni  wa zamu katika hospital ya Bwagala Turiani Lidya mhina akizungumza amethibitisha hospitali imepokea maiti mbili  ambazo si raia wa Tanznai  pamoja na majeruhi mmoja  raia amabye  alifariki muda mfupi wakati akipatiwa matibau  na askari mmoja aliejeruhiwa  amelazwa anaendelea kwa matibabu katika hospitali hiyo.

-ITV

No comments:

Post a Comment