TTCL

EQUITY

Thursday, March 19, 2015

BAKWATA NA MAASKOFU WAPINGANA...


BARAZA kuu la kiislam nchini (BAKWATA) limewataka waamini wote wa dini ya kiislam nchini kuisoma Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba ili kuielewa na kuipigia kura ifikapo tarehe 30, Aprily mwaka huu.

Pichani ni kuu wa Bakwata mkoa
 wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Mussa Salum. (Picha na Maktaba)

Kauli hiyo ya  BAKWATA inakwenda tofauti na Mwamvuli wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, ambalo  ni pamoja na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) ambao wao walitoa tamko ambalo limesomwa kila kanisa wiki hii likiwataka waamini wa dini ya  kikristo kupigia kura ya Hapana katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk. Peter Katula (kulia), akisoma tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania (Picha na maktaba)

Mbali na maaskofu Bakwata wamekwenda tofauti na Jumuiya ya Taasisi za kiislam nchini ambao nao wamewataka pia waamini wa dini hiyo kupigia kura ya hapana katiba hiyo kama haitoitambua Mahakama ya Kadhi.

Kauli ya Bakwata imetolewa jijini Dar es Salaam, na Mkuu wa Bakwata mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Mussa Salum wakati wa Mkutano na Waandishi Habari pamoja na mambo mengine  amesema kwa sasa wao Bakwata hawawezi kuwataka waislam nchini kuipigia kura ya hapana katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.

“sisi tumewataka waamini wa dini ya kiislam nchini kuisoma kwa umakini katiba inayopendekwa na Bunge maalum la Katiba na ikifika wakati wa kuipigia kura waamue wenyewe, maana sisi hatuwezi kuwalazimisha kuipigia kura ya Hapana kama wanavyofanya wengine” amesema. Sheikh Salum ameongeza kuwa kwa kuwataka waislam nchini kuitafuta katiba inayopendekezwa na Bunge maalum.

Katika hatua nyingine Sheikh Salum ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Amani  amemvaa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM, Mhe. Abdurahman Kinana kutokana  na kitendo chake cha kumshambulia Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kwa kumwita waziri huyo ‘eti anazurula tu na wala hafanyi kazi yoyote na kwamba anathamini wanyama kuliko binadamu”

“Kamati  ya amani imesikitishwa sana na kauli  za kinana ambazo zinalengo kumbeza waziri nyalandu katika jitihada zake anazochukua katika kupambana na majangili wa maliasili ya nchi, wanyama ambao wamekuwa wakimaliza wanyama” Ameendelea kusema Sheikh Salum.

Aidha Sheikh Salum amemtaka katibu huyo wa CCM kuacha kumbeza Waziri Nyalandu na akamtaka kuwaangali wakuu wa wilaya pamoja na mikoa ambao wamekuwa na tabia ya kuzurula bila kuwa na mipango yoyote.

      Kamati hiyo ya Amani ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Sheikh Salum pamoja na kuundwa na viongozi mbali mbali wa dini ya kikristo pamoja na dini ya Kiislam.

No comments:

Post a Comment