TTCL

EQUITY

Wednesday, December 24, 2014

Waziri mpya wa usalama aapishwa Kenya

Joseph Nkaissery ndio waziri mpya wa usalama nchini kenya
Waziri mpya wa usalama nchini Kenya, Joseph Nkaissery leo ameapishwa rasmi na kuanza kutekeleza wajibu wake kama waziri akikutoa onyo kali kwa maafisa wa usalama kwamba ni lazima wawajibike la sivyo watimuliwe.
Jenerali huyo mstaafu anasema raia wa Kenya wana haki ya kupata usalama bora zaidi kutoka kwa maafisa wa polisi.
Nkaissery anamrithi Joseph Ole Lenku aliyetimuliwa kazini na rais Uhuru Kenyatta mwezi uliopita. Emmanuel Igunza anaarifu.
Katika hotuba yake ya kwanza punde tu baada ya kuapishwa, Nkaissery amesema anafahamu kuhusu mtazamamo wa umma wa kutokuwa na imani na idara ya polisi nchini.
Lakini amesema anataka kukabiliana na hili kwa dharura kwa kuwahimiza maafisa wote kuwawajibikia wananchi.
Vilevile ameitetea sheria mpya ya usalama iliyoidhinishwa hivi maajuzi nchini ambayo imezusha mjadala mkali. Nkaissery amesema anaamini kwamba sheria hiyo ya kukabiliana na ugaidi ambayo upinzani unaiona kuwa kali inayokiuka uhuru wa wananchi itasaidia zaidi katika kukabiliana na tishio la kundi la wanamgambo wa kiislamu kutoka Somalia, Al Shabaab.
Rais Uhuru Kenyatta amemteua Nkaissery baada ya msururu wa mauaji yaliotekelezwa huko kaskazini mashariki mwa Kenya ambayo kundi hilo la Alshabaab linatuhumiwa kutekeleza. Kundi hilo limetekeleza mashambulio kadhaa ya kigaidi nchini.

No comments:

Post a Comment