TTCL

EQUITY

Wednesday, December 17, 2014

TANZIA: Aliekuwa mneguaji wa muziki wa Bendi Aisha Madinda Afariki Dunia Hii Leo

TANZIA:Aliekuwa mneguaji wa muziki wa Bendi Aisha Madinda Afariki Dunia Hii Leo

     
    Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amethibitisha kutokea kifo hicho na kuongeza kuwa mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar.
    Aisha madinda ambae jina lake halisi ni Aisha Mbegu alizaliwa mwaka 1980 katika  Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar na alipata umaarufu mkubwa kwa uhodari wake wakucheza muziki alipokuwa kwenye  Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta"
    Vile vile Aisha aliwahi kuingia kwenye tasnia hii ya filamu na kuweza kuigiza filamu na watu kama aliekuwa muimbaji wa Bendi ya Msondo, TX Moshi William (Marehemu)  pamoja na mcheza soka Boniphace Pawasa.
    Taarifa zaidi juu ya msiba huu tutaendelea kukujuza kadri tutakapo pata taarifa.
    Pole ziende kwa ndugu na jamaa na wote walioguswa na msiba huu.
    Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema pemoni AMEN.

    No comments:

    Post a Comment