TTCL

EQUITY

Wednesday, December 17, 2014

Kampeni za Kupunguza ajali zaanza Jijini Arusha

Jiji la Arusha limeungana na mkoa wa Dar es salaam na Mbeya katika kampeni za kukabiliana madereva walevi,wanaopiga na kupokea simu wakiwa wanaendesha magari tatizo ambalo limekuwa miongoni mwa vyanzo vya ajali za barabarani zinazoepukika.

Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha, Marison Mwakyoma akizungumza na madereva wa mabasi ya mikoani
Wakizungumza katika uzinduzi wa kampeni hizo Jijini Arusha Mratibu Msaidizi kikosi cha usalama barabarani Mkoani arusha Bw,Emilian Kamhanda pamoja na kushukuru kampuni ya vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu
Nay Mkuu kampuni ya Vodacom Kanda ya Kaskazini wa Bw, Henry Tzamburukaz,amesema wataendelea kutoa ushirikiano wa kukabliana na majanga yanayoepukika likiwemo la ajali za barabarani.
katika uzinduzi huo wafanyakazi wa kampuni ya vodacom wameshirikiana na askari wa usalama barabarani na wajumbe wa baraza la taifa la usalama barabani kuhamasisha na madereva juu ya suala hilo na kuwagawia pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto

No comments:

Post a Comment