Mrembo wa Namibia na mshindi wa Big Brother Africa The Chase, Dillish amemnunulia
mwakilishi wa Ghana kwenye shindano hilo la mwaka jana, Elikem, pikipiki ya kifahari yenye thamani ya dola za Kimarekani 14,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 22 za Tanzania.
Wawili hao walikuwa wameahidiana kununuliana zawadi kama mmoja wapo angeshinda ambapo Dillish alimuahidi Elikem kumpa pikipiki na Elikem alimuahidi mrembo huyo kumnunulia gari kama angeshinda. Na wiki hii Dillish ametimiza ahadi yake kwa kumnunulia pikipiki hiyo aina ya Suzuki GSXR 1000.
Dillish alipost picha ya pikipiki hiyo kwenye Instagram na kuandika: "Finally got my brother the bike he said he would buy if he won. We made a bet on this and I am a woman of my word. Enjoy it buddie and be SAFE!!!"
Elikem alitweet akisema: @Dillish_lishy . thanx hun. U kept ur word. LOVE LOVE all over u".
No comments:
Post a Comment