TTCL

EQUITY

Thursday, November 20, 2014

Mwanamuziki awaudhi Waarabu kwa mavazi

Wanawake kutoka nchi za kiarabu hufunika sehemu kubwa ya miili yao kwa mavazi marefu
Mwanamuziki mmoja mashuhuri wa miondoko ya Pop kutoka Lebanon amekemewa katika mitandao ya kijamii na watu jamii ya waarabu wakiwemo Wanawake.
Wiki iliyopita, muimbaji huyo Haifa Wehbe alitoa burudani ya wimbo katika mashindano ya kipaji cha kuimba kinachorushwa na Televisheni cha nyota wa kiarabu akiwa amevalia gauni refu jeusi lililomkamata barabara maungo yake na linayomuonyesha sehemu za mwili wake.
Zaidi ya Watu milioni mbili walimuona mwanamuziki huyo aliyekuwa jukwaani .Walitazama kwa njia ya Televisheni na intaneti baada ya vipande vya video yake kuwekwa kwenye mtandao wa YouTube.
Watu waliguswa na video hizo hasa wanawake nchini Misri, Jordan na Saudi Arabia, wakakemea vikali namna mwanamuziki huyo alivyochagua mavazi yake.
Maoni kuhusu namna ambavyo mwanamke wa kiarabu anapaswa kuvaa yalionekana kutawala zaidi, huku Lebanon mavazi mafupi ya kubana kwao si hoja.
Katika nchi nyingine mfano Saudi Arabia, wanawake hujifunika nyuso zao na miili yao kwa mavazi meusi , hata hivyo wanawake wamekuwa wakiwafuatilia watu maarufu wakiwa katika hali ya kujificha au katika maeneo wanapokusanyika wanawake peke yao.
Watu wengine wamesifu kile alichokivaa wakisema kila mtu ana uhuru wa kuvaa atakacho, na si mara ya kwanza kwa watu kuvaa nguo zenye kuonyesha maungo.
Dana Khairallah anamiliki blogu ya mitindo, haungi mkono msimamo wa watu dhidi ya mwanamuziki huyo akisema kuwa haya yanakuja kwa sababu ya uwepo wa mvutano kuhusu tamaduni za kiarabu wakidhani kuwa kuvaa hivyo ni kuharibu utamaduni jambo ambalo amesema si kweli. Kisha akahoji kuwa huwa anawaona wasichana wakiarabu wakiwa katika mavazi mafupi yenye kufedhehesha katika kumbi za burudani nyakati za usiku lakini hakuna anayejali kwa kuwa hakuna kamera.

No comments:

Post a Comment