TTCL

EQUITY

Sunday, November 30, 2014

ESCROW:Spika adaiwa kuwalinda washukiwa

Spika wa bunge la Tanzania Anne Makinda
Speaker wa Tanzania Anne Makinda ameshtumiwa kwa kujaribu kuwatetea wale wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi ya Escrow.
Kulingana na wachambuzi,wasomi na wataalam wa sheria hatua yake ya kujenga mazingira ya kuwapendelea washukiwa huenda ikasaidia kuwalinda watu hao.
Wakili maarufu mjini Daresalaam Sylvanus Sylivand ameliambia gazeti la the Citizen kwamba spika makinda alitarajiwa kufuata mfano mzuri uliowekwa na wenzake katika kashfa za awali ambapo bunge lina uwezo wa kuwashinikiza mawaziri na waziri mkuu kujiuzulu.
Ni wazi kwamba bunge linaweza kuishauri serikali kuwachukulia hatua viongozi wanaoshukiwa lakini si lazima kwamba rais afuate agizo hilo.
Kulingana na Sylivand,ni wazi kwamba kuna kitu kinachofichwa ili kuendesha ajenda tofauti ambayo itasadia aibu iliopata serikali.
Bunge la Tanzania
Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma Paul Loisulie amesema kuwa bunge sharti lichukue hatua kama taasisi.
''Kile ambacho kimetokea bungeni kuna uwezekano mkubwa kitaligawanya bunge na wananchi.''.
Inaonekana kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wanajaribu wawezalo kuwatetea viongozi wanaoshukiwa bila kujali maslahi ya raia walio masikini.
Julius Mtatiro wa Chama cha Civic Front amesema kuwa CCM inataka kuwalinda viongozi wake wakuu ili raia wasielewe kuhusu kilichotokea baada ya Spika Makinda kuwataka baadhi ya washukiwa hao kupendekeza hatua ambazo zingefaa kuchukuliwa dhidi yao.
Kulingana na Profesa Kitila wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Wabunge wana uwezo wa kuwaweka katika mizani watu watatu pekee ,rais,waziri mkuu na Spika na kile kilichokuwa kikendelea bungeni ni fursa ya wananchi kufikiria sana kabla ya kuipitisha katiba mpya.

No comments:

Post a Comment