TTCL

EQUITY

Sunday, October 26, 2014

Bawacha yawataka wananchi Bukombe wasikubali kulazimishwa kuunga mkono katiba inayopendekezwa.


Mwenyekiti wa baraza la wanaweke Chadema Halima Mdee amewataka wananchi wa Bukombe mkoani Geita wasikubali kulazimishwa kuunga mkono katiba inayopendekezwa waangalie kama katiba hiyo imezingatia maoni waliyo yapendekeza yakiwemo ya kutaka rasilimali za nchi zilizopo zitumike kunufaisha wananchi wote kwa usawa.

Mdee amesema wakati akizungumza na wanancchi wa Bukombe ambapo amesema baadhi ya masuala yaliyowekwa kwenye rasimu inayopendekezwa yakiwemo ya kilimo, uvuvi, ardhi na mifugo siyo kati ya mambo 14 ya muungano na hayo ndiyo yanafanywa kuwa propaganda ya bunge maalumu la katiba kuwa rasimu hiyo haijazingatia maoni ya watanzania huku ibara ya 22 kifungu cha pili kinamnyima haki mwananchi kudai haki zilizowekwa ndani ya rasimu hiyo mahakamani.
 
Naye mjumbe wa mkutano mkuu wa Bawacha Upendo Peneza  amesema serikali imeshindwa kusimamia na kulinda rasilimali za watanzania kwa baadhi ya wawekezaji wanaochimba madini katika migodi ya mkoa wa Geita bila kulipa kodi kwa madai watahusika katika kufanya shughuli za maendeleo zikiwemo kujenga shule na zahanati huku wachimbaji wadogo wakiendelea kunyanyasika kwa kulipa kodi na  kushindwa kujiendeleza kiuchumi.

No comments:

Post a Comment