TTCL

EQUITY

Wednesday, September 24, 2014

Picha: Hamisa Mabeto amuanika mchumba wake

Mwanadada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto ameamua kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya kijamii  huku akimmwagia sifa kemkem.
Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili baada ya kuvutiwa waya, Hamisa alisema mwanaume huyo ni mtu ambaye anampenda sana na wana malengo ya kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka hadharani soon!
Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.

 Hamisa Mabeto katika pozi.
“Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,” alisema Hamisa.

Mwanadada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto akila ujana na mpenzi wake.
Mwanadada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto akila ujana na mpenzi wake

No comments:

Post a Comment