TTCL

EQUITY

Friday, April 18, 2014

UCHAFU WA MAZINGIRA NA ATHARI ZAKE

urundika taka taka kihorela katika mitaa yetu
Mazingira ni vitu vyote vile vinavyotuzunguka katika maisha tunaoishi ama  maeneo tunayoishi. Mazingira yanaweza kumfanya mtu kuwa katika afya iliyobora na isiyo bora kuwa na afya bora, pamoja na kuendelea kuwa na afya bora ni wajibu wa kila binadamu.Tunahitaji kuwa na miili yenye afya bora na nguvu ili tuweze kuendelea na shughuli zetu za kila siku katika ujenzi wa wa Taifa. Kila binadamu ana marengo aliyojiwekea katika maisha na ili marengo hayo yatimie ni lazima mwanadamu huyo awe na afya iliyo bora zaidi. Ni wazi kabisa katika nyakati hizi, na katika jamii tunayoishi, kiwango cha usafi wa mazingira ni duni sana na hamna viwango maalum vilivyowekwa katika kuyaweka mazingira safi.
Nadhani kitu kikubwa kinachotufanya tuwe hivi na kutojali kuyaweka mazingira yetu yawe safi, ni mazoea tuliyokuwa nayo na tumekulia katika mazingira yasiyo safi hali iliyotufanya tuzoee mazingira yasiyo safi. Tazama vyakula vinavyouzwa mtaani bila kufunikwa katika vumbi jingi na moshi mzito utukanao na magari na shughuli nyingine, lakini tunanunua na kula.  Ni ukweli kuwa ulaji huo hupelekea kupata magonjwa ambayo hutufanya tujikute katika hospitali mbali mbali tukihangaika kuokoa maisha yetu. Ni gharama kwetu na gharama kwa Taifa kwa ujumla.
Tazama wasafiri wa vyombo mbalimbali vya majini, mijini, katika mikoa na hata nje ya nchi watupavyo taka katika mazingira bila kujali uharibifu, bila kujali kama ni mbuga ya wanyama,  kama ni chanzo cha maji na hata bila kujali kama ni msitu wa hifadhi.

Kama hatutatupa takataka au kuziharibu katika njia iliyo sahihi, tutapata magonjwa mbalimbali hatari yanayotokana na utupaji ovyo huo. Tunaweza kugawanya aina ya taka katika makundi makuu matatu.

1)         Taka za kawaida za nyumbani, ambazo nazo zimegawanyika katika taka ngumu(plastiki,glasi, bati,mbao nk)  taka laini za jikoni(mabaki ya chakula), na maji taka(kutoka katika vyoo na mabafu).

2)   Taka za viwandani kama maji taka na kemikali mbalimbali pia taka ngumu.

3)  Taka za Hospitali ambazo nazo zinahitaji uangalizi mkubwa kuepuka kusambaa kwa magonjwa mbalimbali.

Taka zinazoharibu vyambo vya maji
Asilimia kubwa ya watu hawana mazoea ya kutupa na kuhifadhi takataka katika njia iliyo sahihi na salama, ni kawaida kukuta taka za majumbani na hata viwandani zikiwa zimezagaa ovyo kwenye mitaa, barabarani, majengo ambayo hayatumiki, katika mitaro, mtoni,chini ya madaraja. Pia kwenye vyanzo mbali mbali vya maji kama bahari, mito na maziwa na ikiwa maeneo haya ndiyo watu wengi hutumia maji haya kwa matumizi ya nyumbani na hata kunywa. Uwepo wa taka hizi umelekea kuwepokwa harufu mbaya na kali zaidi mpaka imekuwa kero kubwa kwa mtu kuishi kutokana na kuepo kwa mrundikano wa taka  ambazo zinawaathiri kiafya wakazi wa maeneo hayo.
Taka zinazozalishwa na familia zaweza kuwa hatari zisipotupwa na kuharibiwa katika njia iliyosahihi. Taka hizi zaweza kupelekea milipuko ya magonjwa hatari, na zinapoachwa wazi zinaweza kuchafua mazingira, na kusambaza magonjwa kupitia upepo unaovuma, wadudu kama inzi na mende, na pia uambukizo wa magonjwa waweza kusambazwa kupitia njia ya upumuaji. Vimelea vya magonjwa vyaweza pia kuingia katika vinywaji visivyofunikwa, vyakula vilivyoachwa wazi barabarani na kusababisha magonjwa kama kuhara damu, kipindupindu, homa ya tumbo, minyoo, kichefuchefu na kutapika.

Kutunza mazingira na yakawa safi ni jukumu la kila mtu bari si la serikari pekee kwasababu kila mtu anahitaji awe na afya bora na kuwa na ili uwe na afya bora ni lazima mazingira yanayokuzunguka yawe safi. Kwa hiyo basi, kuyaweka mazingira yetu katika hali ya usafi, kutatuepusha na matatizo mengi yakiwemo magonjwa mbali mbali ya mlipuko.

No comments:

Post a Comment