Ijumaa
ya leo msanii alietoka kwenye familia ya Super Nyota wa mwaka 2012
Young Killer amepiga dua maalum kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha
kuanzia alikotoka mpaka alipo sasa ambapo kwenye dua hiyo iliyofanyika
kwa saa mbili, Killer pia aliwaalika ndugu jamaa na marafiki kwa ajili
ya chakul nyumbani kwake Kinondoni.
Anasema ‘nimeamua kusoma dua hii maalum na kumuita Shekh ili kumshukuru Mungu kwa kila nifanyacho na baraka zake nikaona sio vibaya nikitumia nafasi hii pia kuwaalika ndugu zangu kujumuika nao katika dua hii muhimu’-Young Killer
Waalikwa wa dua hii walikua ni wale kutoka familia yake anayoishi nayo Classic Sound pamoja na majirani wa nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment