TTCL

EQUITY

Tuesday, November 12, 2013

SKENDO YA PICHA CHAFU ZINAZOMUONESHA MH LEMA "FAKE" AKIFANYA UCHAFU NA MWANUME MWENZAKE..!YEYE MWENYEWE NA MKEWE WAELEZA UKWELI, SOMA HAPA!

Mbunge wa Arusha mjini Godbles amekanusha  na kukemea vikali baadhi ya watu wanaomdhalilisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kutengeneza na kusambaza picha chafu ambazo zinaonesha udhalilishaji mkubwa kwa mbunge na hata kwa mtu wa kawaida.
Akizungumza  na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Arusha mbunge Lema amesema picha hizo za aibu zimetengezwa na kusambazwa na mtu ama watu wenye lengo la kumdhalilisha na tayari amekwishaanza hatua ya kuchukua hatua za  kufikisha suala hilo kwenye uongozi wa bunge akiwemo Spika Anne Makinda, naibu spika Job Ndugai pamoja na katibu wa bunge.

Amesema ameamua kutoa taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari kwa sababu vitu vikishawekwa kwenye mitandao ya kijamii siyo siri tena hivyo anategemea bunge litaona wajibu na ni jinsi gani heshima ya mbunge imeshushwa na kudhalilisha kwa maksudi bila kujali utu na heshima ya mbunge.

No comments:

Post a Comment