TTCL

EQUITY

Thursday, November 14, 2013

DOGO ISMAIL: DOGO HUYU ANASIFIKA KWA KUPIGANA NA WALIMU..!! SOMA HAPA UMFAHAMU..!!

http://theclicktz.blogspot.com/
Kitaani huyu dogo anajulikana kama dogo ismail, ni maarufu sana mtaani kwao huko Yombo. Dogo Ismail anishi na mzazi wake mmoja wa kike huko Yombo na mama yake anafanya kazi kwenye kampuni fulani ya usafi hapa jijini.
Dogo Ismail amemaliza darasa la saba mwaka huu 2013, huko huko Yombo alipokuwa akiishi yeye na mama yake, lakini dogo huyu anasifa yake moja kuu ya ugomvi. Wakati akiwa bado shule alikuwa akiwaletea sana utata walimu na wakati mwingine hata kushikana mashati na kupigana, alishawahi kumpiga jiwe mwalimu mkuu akiwa mstalini, dogo alirudishwa nyumbani kwa muda fulani na baadae alirudishwa shule, Mama yake Bi. Mariam akiendelea kuileza unbounderies news
Mtoto wake alidhaniwa kuwa labda anamatatizo ya akili, lakini yeye mwenyewe anakanusha huku akisisitiza kuwa mwanae yuko sawa kabisa ila ni utoto tu kwani wakati mwingine  watoto huwa hivyo na wanapokuwa hubadilika na kuwa wema kabisa, na akiongezea kuwa Ismail anapo kuwa nyumbani ni mtulivu sana hivyo anashangaa matukio anayoyafanya huko nje.!!
Kwa mujibu wa watoto wenzake wa kitaa wanadai kuwa Ismail ni mgomvi sana, na huwa anashindaga kwenye kibanda fulani cha video hapo kitaani mara tu anapotoka shule na kurudi nyumbani kwao jioni hivyo labda huko ndiko anakopata maujuzi ya ugomvi na kujifanya stelingi wakati wote.

No comments:

Post a Comment