Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa nchini Mali ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa maafisa wa Ufaransa, mwanajeshi
huyo kutoka kikosi maalum cha Ufaransa aliuawa Magharibi mwa nchi baada
ya gari lake kulipukiwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara.
Hadi kufikia sasa wanajeshi sita wa
Ufaransa wameuawa tangu Ufaransa kuanza operesheni yake dhidi ya
wapiganaji wa kiisilamu waliokuwa wanadhibiti Kaskazini mwa nchi
Ufaransa ilitangaza kuanza kuondoa baadhi ya wanajeshi wake 4,000 walioko Mali.
Lakini wengine 1,000 watasalia nchini humo hadi
mwakani kuweza kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu walio na uhusiano
na kundi la Al-Qaeda
Baadhi ya miji, imeweza kudhibitiwa na wanajeshi
hao, lakini wapiganaji hao wangali kwenye maficho yao ya mwisho
Kaskazini mwa Mali ambako wanafanya mashambulizi ya kuvizia dhidi ya
wanajeshi wa Mali na Ufaransa.
Hivi maajuzi Umoja wa Mataifa uliafikia kunda kikosi cha wanajeshi 12,000 kushika doria nchini Mali.
Watashirikiana na kikosi cha wanajeshi 6000 ambao tayari wako nchini humo.
Rais Francois Hollande ametoa rambi rambi zake kwa familia za waliouawa huku akiwasifu kwa ujasiri wao nchini Mali.
No comments:
Post a Comment