Viongozi wa Tanzania na Zanzibar
walikuwa miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria mazishi ya mwanamuziki
mkongwe wa Kisiwani Zanzibar Fatma binti Baraka, aliyesifika kama Bi
Kidude.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema kuwa watu wengi, walikuwa na majonzi kwani wengi walimuona kama bibi au nyanyaoInaaminika alikuwa na zaidi ya miamoja na alikuwa mtumbuizaji wa nyimbo za Taarabu
Aliendelea kutumbuiza wengi licha ya umri wake.
Mnamo mwaka 2005, alituzwa kwa mchango wake katika fani ya muziki wakati wa mkusanyiko mkubwa wa wanamuziki duniani
Mamia ya wanawake waliomboleza nyumbani kwake kabla ya mwili wake kupelekwa kwa maombi kisha mazishi.
Alizikiwa kijijini kwao Kitumba, ambako rais Jakaya Kikwete alitoa heshima zake za mwisho.
Duru zinasema Bi Kidude alitumbuiza wengi na watu walimpenda kwa miondoko yake.
Inaarifiwa Bi Kidude alianza kuimba taarabu mwaka wa 1920
Siku rasmi ya kuzaliwa kwa Bi Kidude haijulikani lakini kuna tetesi liwa alizaliwa mwaka 1910.
No comments:
Post a Comment