Walimu
wapya wanaochelewa kupata mishahara yao kwa wakati ni wale ambao kwa
sababu zao wanakwepa kwenda kwenye vituo wanavyopangiwa na Wizara na
kuripoti wanapotaka wao.
Hayo
yamebainishwa leo na Waziri wa Utumishi, Mhe. Celina Ompeshi Kombani
wakati akifafanua Bungeni suala la kuchelewa kwa mishahara ya Walimu
shule za vijijini lililoulizwa na Mhe. Riziki Omar Juma (Viti Maalum).
Mhe.
Kombani amesema baadhi ya walimu kwa makusudi huwa hawaendi kwenye shule
wanazopangiwa na hivyo majina yao hayaonekani katika orodha ya shule
wanazoamua kwenda ambapo mishahara yao hupelekwa katika vituo
walivyopangiwa na hivyo walimu hujikuta wanachelewa kupata mishahara
yao.
Katika
jibu la msingi lililotolewa na Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (Elimu) Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wa kuhusu swali hilo
amesema kuwa serikali huwahudumia walimu wapya wanaoajiriwa bila kujali
wamepangwa katika shule za vijijini au mjini ikiwemo kulipwa mishahara
na staili zao nyingine.
Amesema
mishahara kwa waajiriwa wote wapya hulipwa baada ya mwajiriwa kujaza
fomu za ajira na kuwasilisha taarifa binafsi ikiwemo vyeti vya taaluma
na kitaalamu.
Baada
ya hatua hizo, Halmashauri husika huziingiza katika mfumo wa malipo
ambao hupeleka moja kwa moja majina hayo kwa njia ya mtandao Ofisi ya
Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma, kwa ajili ya kuidhinishwa na
maandalizi ya malipo ya mishahara kwa mwezi unaofuata.
Amesema wanaochelewa kupata mishahara ni wale ambao majina yao huchelewa kutuma baada ya tarehe Nane ya mwezi.
Mhe.
Majaliwa amesema mwalimu akichelewa kupata mshahara na yupo kituoni,
Mkurugenzi wa Halmashauri anawajibika kumuhudumia ili aweze kujikimu.
Amesema
Serikali imekuwa ikituma fedha za posho katika Halmashauri kabla ya
walimu kuripoti katika juhudi za kuboresha mazingira ya kazi kwa
watumishi ikiwemo walimu.
Hata
hivyo amekiri kuwepo na maeneo nchini ambayo mtandao hufanya kazi
taratibu na hivyo husababisha baadhi ya walimu kutoingia katika orodha
ya malipo kwa wakati na kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha
walimu wote ambao hawajaingizwa katika orodha wanahudumiwa ipasavyo.
No comments:
Post a Comment