TTCL

EQUITY

Thursday, April 18, 2013

BASI LA MGHAMBA TOKA KAHAMA KWENDA ARUSHA LAGONGA NA KUUWA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI TINDE MKOANI SHINYANGA.


SAMAHANI KWA PICHA HII JAMANI.

Mwili wa Marehe Grace Bernad muda mchache baada ya kugongwa na gari.

Mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Grace Benard mkazi wa kijiji cha Jomu wilaya ya Shinyanga vijijini anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Tinde amefariki baada ya kugongwa na gari la abiria.

Mtoto huyo amegongwa asubuhi ya leo  katika kijiji cha Tinde na basi la kampuni ya Mghamba ya jijini Arusha yenye namba za usajili T424 AWB iliyokuwa ikiendeshwa na Bakiri Rajabu(42) mkazi wa Arusha.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa ajali hiyo imetokea kufuatia mtoto huyo kuvuka barabara akitokea nyuma ya roli wakati basi hilo likiwa katika mwendo.

Mganga mkuu msaidizi wa kituo cha Afya Tinde amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ili kusubiri taratibu za mazishi.

Kufuatia tukio hilo wananchi wa kijiji cha Tinde wakishirikiana na wanafunzi wa shule hiyo walifunga barabara kuu itokayo Mwanza kuelekea Dar es salaam kwa saa nne wakiishinikiza serikali kuongeza matuta katika eneo hilo.

Sambamba na hayo wananchi hao walikaidi agizo la Diwani wao pamoja na Jeshi la Polisi kuondoka na kuondoa mawe barabarani hadi pale kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) kutoka mkoani Shinyanga kilipotumia mabomu ya Machozi.
MATUKIO KATIKA PICHA


 
Wnafunzi pamoja na wananchi wa kijiji cha Tinde wakiuangalia mwili wa marehemu
 
 
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiufuniki mwili wa marehemu ili kuusitiri.
 
Wnanchi wakitaaruki juu ya kifo cha mwanafunzi huyo kilicho sababishwa na ajali ya basi.
 
Gari la wagonjwa kutoka hopitali ya mkoa shinyanga ikiwa imewasilieneo la tukio ili kuuuchukua mwili wa marehemu.
 
MAANDALIZI YA KUUPAKIA MWILI WA MAREHEMU.

Wanafunzi wa shule ya msingi Tinde wakikusanya mawe na kufunga barabara.

Wanafunzi wakifanya maandamano ya kudai  kuwekwa kwa matuta ya kupunguza mwendo kasi.
 
Na huu ndio mwonekano wa barabara mara baada ya kufungwa kwa mawe.

Wnanchi wakishiriki kuwaunga mkono wanafunzi kufunga barabara kwa kukaa barabarani.



Magari yakiwa yamekosa pakupita mara baada ya barabara kufungwa kwa mawe
 
FFU wakiwasili katika eneo la tukio kwaajili ya kuweka usalama.

Jeshi la polisi FFU na Usalama barabarani wakituliza fujo
za wananchi walio kuwa na hasira kali.

Wanafunzi wakina masononeko ya kupotelewa kwa mwenzao
aliyegongwa na gari na kukutwa na mauti.
 
Askari wakipanga mikakati ya kuwatawanya wananchi.

BASI LA MGHAMBA LIKIWA LIMEPAKI KITUO CHA POLISI TINDE

No comments:

Post a Comment