Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba
hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Kamati ya Fedha ya
Bunge la Finland.
Katika
mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Luthuli
Dar es Salaam, wabunge hao wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa
jitihada inazofanya za kulinda na kuhifadhi mazingira.
Awali,
akiwakaribisha wabunge hao Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia
uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Finland na kuwashukuru
wabunge hao kwa kufanya ziara hiyo ya kikazi nchini Tanzania.
Waziri
Makamba amesema Serikali ya awamu ya Tano imejikita zaidi katika
kuimarisha Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa
Mkakati Mkubwa wa Kitaifa wa kupanda miti nchi nzima hususan maeneo kame
ili kunusuru nchi na athari za mabadiliko ya Tabianchi.
“Hivi
sasa tuko katika hatua za kuainisha maeneo yatakayopandwa miti hiyo kwa
kuangalia aina za udongo na miti itakayoweza kuhimili katika maeneo
husika” Alisisitiza Makamba.
Waziri
Makamba ameiomba Serikali ya Finland kuendelea kushirikiana zaidi na
Serikali ya Tanzania ili kufikia malengo endelevu ya Uchumi na maendeleo
ya Viwanda bila kuathiri Mazingira.
Naye
Balozi wa Finland Nchini Tanzania Bw Mart Akhtsary aliyeambatana na
ujumbe wa wabunge kutoka Finland amemhakikishia Waziri Makamba
kuendeleza na kudumisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) January
Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge la Finland.
Wabunge hao wa Kamati ya Fedha wamefanya mazungumzo na Waziri Makamba
hii leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment