Na Ferdinand Shayo Arusha.
AfisaMaendeleo ya jamii Mkoa wa Arusha Blandina Nkini amesema kuwa watoto
wengi hupata mimba kipindi cha likizo za mashuleni kutokana na ufuatiliaji
mdogo wa wazazi kwa watoto wawapo mashuleni na majumbani hali inayochangia
ongezeko la mimba za utotoni na kuzorotesha elimu.
Blandina alisema
kuwa uzoefu unaonyesha kuwa wazazi wengi hawana muda wa kukaa na watoto wao kuzungumza na wanao juu ya maadili pindi
wanaporejea kutoka shule za bweni.
Afisa huyo
akizungumza katika mkutano wa kujadili mipango ya mwaka 2016 /17 ya shirika
lisilokua la kiserikali la The Foundation For Tommorrow linalojihusisha na
masuala ya watoto ,amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto hasa
kipindi ambacho wanakua likizo ili kuwajengea uwezo juu ya changamoto za ukuaji zinazowakabili na namna ya
kuzitatua.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika Hilo Melisa Queyquep amesema kuwa kwa sasa wana mpango wa kutoa mafunzo kwa kwa walimu 500 kwa miaka 5 .
Melisa
alisema kuwa wameanzisha mpango huo mahususi
ili kuwezesha upatikanaji wa walimu bora kwani vigumu kuwa na elimu bora
bila kuwa na walimu bora.
“Kwa sasa
tunasomesha watoto 114 wanaosoma kwa
ufadhili kwa kipindi cha mwaka huu na
pia wanatarajia kuwafikia watoto wengi wa kitanzania ambao ni yatima na
wanaishi katika mazingira magumu” Melisa
Mkurugenzi
Mkazi wa shirika hilo aliyemaliza muda
wake Arusha Kennedy Oulu alisema kuwa serikali inapaswa kuboresha elimu mbali
na kujenga majengo pia madawati,vyoo na
vifaa vya kufundishia vitiliwe mkazo.
No comments:
Post a Comment