ljumaa
Kuu ni siku ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha
kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu
siku ya Ijumaa.
Kadiri
ya Mtume Yohane kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka, jambo
lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali
wanakadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.
Ijumaa
kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji
huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaaniMasiya au Kristo).
Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi.
Ijumaa
kuu ni pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na
kifo chake, kulala kaburini, na hatimaye kufufuka kwa utukufu
Siku tatu kuu za Pasaka ndizo kiini cha mwaka wa Kanisa.
Zinamuadhimisha
Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, yaani siku ya kwanza (Alhamisi kuu
jioni hadi Ijumaa kuu jioni) inaadhimisha mateso yake kuanzia karamu ya
mwisho hadi kifo cha msalaba; siku ya pili (Ijumaa kuu jioni hadi
Jumamosi kuu jioni) inaadhimisha maiti yake kubaki kaburini na roho yake
kushukia kuzimu; siku ya tatu (kuanzia Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili
ya Pasaka jioni) inaadhimisha ufufuko wake mtukufu.
Siku hizo tatu ni kama bawaba kati ya Kwaresima na kipindi cha Pasaka
No comments:
Post a Comment