WATU
wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mkoani Kigoma, watapata faraja kubwa
mapema Aprili 4 hadi 9, 2016, kufuatia uwepo wa huduma za uchunguzi wa
maradhi hayo utakaofanywa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, Dkt.
Stephan P. Masatu, kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam, Dkt. Masatu alisema,
huduma zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na vipimo vya ECG na
ECHO zitatolewa kuanzia asubuhi kwenye hospitali ya kibinafsi ya Upendo
iliyo jirani na soko kuu la mkoani Kigoma.
Mkoa
wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi na
zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa kushughulikia magonjwa kama ya
Moyo na kutokana na uchache wa wataalamu hao, itakuwa ni nafasi nzuri
kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na vitongoji vyake, kujitokeza ili
kuhudumiwa ambapo kliniki hiyo itadumu kwa muda wa siku sita mfululizo.
DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu.
Dkt. Masatu akitumia mashine ya kupima ECHO, mmoja wa wagonjwa wa moyo.
No comments:
Post a Comment