Ameyasema
hayo alipokuwa akizungumzia suala la upatikanaji wa Meya wa jiji la Dar
es salaam ambapo limegubikwa na mambo ya siasa zizizofaa kwa maendeleo
ya wananchi na wapenda demokrasia nchini.
''Kauli za mvutano na malumbano ya UKAWA na chama cha mapinduzi
havitasaidia wananchi kwanza wanajidhalilisha kinachotakiwa ni upinzani
kutumia busara lakini chama tawala pia watambue kwamba walipokubali
mfumo wa vyama vingi lazima wakubali mabadiliko na kuheshimu mfumo wa
vyama vingi”
Hakuna sababu ya msingi ya kuwepo malumbano hadi watu wengine wapigwe
na wengine kuwekwa rumande kwanza kazi kubwa ya umeya ni kuongoza vikao
ingelikuwa tunatafuta mkurugenzi hapo sawa lakini hili wanakosea kwa
kweli''-Amesema Dkt. Bana
Meya wa jiji la Dar es salaam ameshindwa kuchaguliwa mara kadhaa
pamoja na kuwepo kwa uhalali wa kufanyika uchaguzi huo jambo ambalo
limesababisha malumbano makali na kushikiliwa kwa wabunge wawili wa
Chadema Saed Kubenea na Halima Mdee.
No comments:
Post a Comment