Model mlemavu ateka hisia za wanamitindo wa kimataifa
Baadhi ya watu wenye ulemavu katika miili yao wamekuwa ni watu wa
kukata tamaa na wengine kujikuta wakiwa ombaomba kutokana na kukosa
mahitaji muhimu na hivyo kujikuta wakiwa tegemezi.
Model Kanya Sesser. mwenye umri wa miaka 23 ameonesha kuwa walemavu wanaweza kuushangaza ulimwengu endapo watapata nafasi, na ndio maana mrembo huyo amejikita katika mitindo bila kujali ulemavu alionao.
Sesser, mwenye ulemavu wa miguu anayeishi nchini Thailand, amekuwa akijiingizia kiasi kikubwa cha fedha kwa siku kama mwanamitindo kupitia nguo za ndani za wanawake.
Mrembo huyo kutokana na ulemavu aliozaliwa nao wa miguu alijikuta akitengwa na familia yake na hivyo kulelewa na familia nyingine ambapo akiwa na miaka 15 alijiingiza katika mambo ya mitindo.

Sesser, amedai kuwa hajutii kuwa mlemavu na ndio maana ameamua
kujikita kwenye mitindo ambapo amedai kuwa ameingia mkataba na makampuni
makubwa nchini kama Volcom, Nike na Rip Curl Girl, huko Los Angeles
ambapo kwa siku huingiza zaidi ya kiasi cha dola 1000.
Sambamba na hilo mwanamitindo huyo ni mwanariadha na sasa inadaiwa
kuwa yupo katika maandalizi ya kushiriki mbio za walemavu
zitakazofanyika Korea Kusini mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment