Aliyekuwa mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito (kulia).
Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO)
Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji
mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa
zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya
kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za
serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli
ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge”
Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais
Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa
haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni
hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika
Aidha Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi
Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya
uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.
Pia ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA)
kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa
zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika
ukiukwaji wa sheria.
Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja
bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na
jinsi bodi hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa
ununuzi wa mabehewa ya treni.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
No comments:
Post a Comment