TTCL

EQUITY

Thursday, June 4, 2015

Viongozi TFF wateuliwa wajumbe kamati CAF

Shirikisho la mpira barani Afrika CAF limewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbalimbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.

Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni Leodeger Tenga ambaye atakuwa Makami Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Vyama Wanachama) huku Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Jamal Malinzi akiwa Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20.
Kwa upande wa Mwesigwa Selestine ambaye ni katibu mkuu wa TFF ameteuliwa kuwa mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17 huku Richard Sinamtwa akiteuliwa kuwa Mjumbe Kamati ya Rufaa na Dr Paul Marealle akiteuliwa katika nafasi ya mjumbe Kamati ya Tiba.
Kwa upande wa Lina Kessy ameteuliwa kuwa Mjumbe ya Soka la Wanawake huku Crescentius Magori akiwa Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani.

No comments:

Post a Comment