TTCL

EQUITY

Wednesday, June 3, 2015

HATUA ZA UOKOAJI CHINA KWA WALIOPATA AJALI YA MELI INAENDELEA.

Vikosi vya uokoaji tayari vimeelekea kwenye eneo la tukio

meli hiyo iliwa imebeba  watu wapatao 456 ambapo inaarifiwa zaidi ya watu Watu saba wamethibitika kufa na wengine 14 wamekutwa hai katika, baada ya meli waliyokuwa wakisafiria kukumbwa na upepo mkali katika Mto Yangtze kusini mwaChina na imezama.
Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua watu wanane wameokolewa mpaka sasa na kazi inaendelea ya kuwaokoa abiria wengine.
Waziri Mkuu Li Keqiang anaelekea katika eneo la tukio.
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mashariki mwa mji wa Nanjing kwenda Chongqing kusini magharibi ilipozama.
Meli hiyo, Dongfangzhixing - au Nyota ya Mashariki - ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa shirika la usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.

Wafanyakazi wa uokoaji wakiwa karibu na eneo ilipozama meli

ka miongoni mwa mamia ya waliokumbwa na mkasa wa kuzama kwa meli katika mto Yangtze kutokana na hali mbaya ya hewa.
Maelfu ya waokoaji walifanya kazi usiku kucha katika meli hiyo iliyopinduka ijulikanayo kama "Nyota ya Mashariki" katika jimbo la Hubei.

Ndugu waliojawa na hasira wanalalamikia kukosekana kwa taarifa za uokoaji.
Watu walionusurika ni pamoja na nahodha wa meli na mhandisi mkuu, wote wawili wakiwa katika mahabusu za polisi.
Nahodha amesema meli hiyo ilikumbwa na kimbunga na kuzamishwa chini ya mto katika dakika chache.

Nahodha na mhandisi mkuu, ambao ni miongoni mwa waliokolewa wamekaririwa wakisema kuwa meli ilikumbwa na kimbunga na kuzama haraka.
Kazi ya uokoaji imekwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa. Meli hiyo ilizama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.
Waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Shanghai.
Habari zinasema meli hiyo imepinduka.
Watu ishirini na wawili waliufa katika mto huo mwezi Januari, wakati boti iliyokuwa katika majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang, katika jimbo la Jiangsu.

No comments:

Post a Comment